JE SABUNI NI KIUATILIFU (DAWA YA WADUDU)
JE SABUNI INAWEZA KUTUMIKA KAMA KIUATILIFU????
Na Abbas Mpinga Agronomist (Kilimo Expert)
+255757139423
SABUNI ni Moja Ya Viuatilifu salama kwa binadamu kwasababu inauwezo wa kuuwa wadudu jamii ya vidukari kwa njia ya mguso na mfumo kwa ufanisi saana bila ya kuwa na madhara hasi kwa Afya ya binadamu
Sabuni ina Kiambata cha Sodium au potassium Hydroxide (Na/KOH) ambayo ni very Alkaline compound
Alkalinity yake si rafiki kwa wadudu wasumbufu shambani (Crop pest) hivyo ikitumiwa kwa wadudu hususani vidukari huweza kuwauwa kirahisi saana
- Sabuni huathiri membranes ya seli ya mdudu
- Sabuni huathiri mfumo wa upumuaji wa mdudu
- Sabuni huathiri na kuharibu gamba la ngozi ya mdudu
- Sabuni huingilia mfumo wa homoni wa mdudu
Hii ni kwasababu pia Sabuni ina kinatishi (sticker) ambacho hurahisisha ufanyaji kazi wa Sabuni (NaOH) kama kiuatilifu
Hii ni maarufu pia kwa wakulima na wadau ww viuatilifu duniani, Ili kiuatilifu kifanye kazi kwa urahisi, ufanisi na uharaka bhasi huchangwanywa na kinatishi (stickers) kwa uwiano maalumu!
Mfano wa vinatishi viuzwavyo madukani ni BIDDIQUAT Na OSHO QUAT
MCHANGANYO(application rate): Waweza changanya gram 250 za sabuni ya unga au 250mls za sabuni ya maji kwenye lita 20 za maji
Wasiliana nasi kwa ushauri wa kilimo
+255757 139423 Abbas Mpinga
kilimoforlife@gmail.com
Sante sana @kilimoforlife kwa maelezo mazuri ya matumizi ya sabuni kama kiuatilifu maana sumu zimekuwa hatari .
JibuFutaKaribu
JibuFuta