FAHAMU SABABU YA NYANYA KUDODOSHA AU KUPUKUTISHA MAUWA

SABABU ZA ZAO LA NYANYA NA HOHO KUPUKUTISHA AU KUANGUSHA MAUWA.

KILIMO FOR LIFE ni moja ya mtandao wa kilimo unaoongoza kwa kusomwa na kupitiwa na wasomaji na waperuzi wengi zaidi.

BONYEZA HAPA KUNUNUA FORMULA ZA MBOLEA KWENYE MAZAO

Ni mtandao ulioanzishwa na Mr A. Mpinga mwenye nia,dhamira
na malengo ya kumsaidia Mkulima kunufaika na fursa ya kilimo kwa kumuwezesha kufahamu mbinu na namna bora zaidi ya kukiendea kilimo cha kitaalamu kwa kufuata Kanuni bora zaidi za Agronomia na Matumizi sahihi ya mbolea na viuatilifu pia kutoa tathmini ya gharama za kilimo cha mazao mbalimbali.

Kilimo for life ikiendesha mafunzo kwenye vikundi vyakilimo mkoani Iringa

Imeandaliwa na Mr Mpinga +255 757 139 423
Habari Mpendwa msomaji wa makàla zetu za kilimo cha mazao mbalimbali kupitia mtandao wetu wa Kilimo for life.

Hapa tutaainisha sababu  za tatizo mtambuka ambalo linawasumbuwa wakulima wengi juu ya kupukutika na kuanguka kwa mauwa ya nyanya na pilipili Hoho  shambani kabla au kipindi cha uzalishaji.

BONYEZA HAPA KUSOMA MAKALA YA KILIMO BORA CHA ZAO PILIPILI HOHO. http://www.kilimoforlife.com/2019/06/muongozo-mfupi-kilimo-bora-cha-pilipili.html?m=1

1. NYUZI JOTO 
Kuzidi kwa joto ridi la usiku au mchana ni moja ya sababu kuu ambazo ndivyo visababishi vya mauwa kudodoka kabla ya uzalishaji.
Utafiti unaonesha kuwa, kupanda kwa joto la mchana zaidi ya nyuzi joto 40 °C husababisha mauwa kuanguka.
Pia kupanda kwa joto la usiku zaidi ya nyuzi joto 35° C na kushuka kwa joto la usiku chini ya nyuzi joto 25°C husababisha mauwa mengi kuanguka kabla ya uzalishaji wa matunda.

Poa utafiti unaonesha kuwa: Joto la mchana likizidi zaidi ya nyuzi joto 48° C kwa muda wa siku 4, Husababisha mmea kuangusha mauwa ili kuepusha kuzalisha bali kujiongezea fursa na uwezo wa kustahimili hali ngumu na kuepusha.

BONYEZA HAPA: KUFAHAMU TATHMINI YA GHARAMA ZA KILIMO CHA NYANYA 

Hata hivyo utafiti unaonesha kuwa, kushuka kwa nyuzi joto wakati wa usiku chini ya nyuzi 25°C hufanya tube ya poleni (Pollen tube) kushindwa kukuwa, hivyo kufanya kushindikana kwa uchafushaji (Fertilization) kutokea.

Pia Joto linapozidi zaidi ya nyuzi joto 40°C hukausha  poleni katika mauwa, hivyo kushindikana uchafushaji (Pollination failure).
Baada ya hapo poleni hukauka na hatimae mauwa huanguka kwa kupukutika.

2. Hali ya Unyevu shambani (Relative Humidity) : kwa kawaida Hali ya Unyevu katika shamba la nyanya inapaswa kuwa 40% hadi 70%.

MBEGU BORA ZA TIKITI, VITUNGUU, NYANYA, HOHO, N.K 

Endapo Hali ya unyevu (RH) shambani ni ndogo saana, hupunguza uwezekano wa poleni kuchavusha, kwani poleni huwa kavu kupita kiasi. Na endapo Hali ya Unyevu shambani ni kubwa zaidi hufanya poleni kushindwa kunatana (kuchavusha) vizuri kipindi cha uchavushaji.

3. Kiwango cha Nitrogeni:
kuzidi kwa virutubisho vya Nitrogeni shambani na kwenye mmea; hufanya mmea kuzalisha majani zaidi kuliko kuelekeza nguvu kwenye mauwa na matunda.

HIVYO MKULIMA ASIVUTIWE NA UKIJANI WA MMEA WAKE.

4. Uzalishaji mkubwa zaidi wa matunda katika mmea:
pindi shina linapozalisha matunda mengi zaidi, hufanya matunda kugombania virutubisho, hivyo mmea hatimae huangusha baadhi ya matunda ili kuweka usawa wa usambazaji ama ugawaji wa virutubisho.

5.Upepo:
upepo mkali na wenye nguvu, huangusha mauwa na kupunguza utengenezwaji wa mauwa na matunda.

6. Mwanga wa Jua: 
Kukosekana kwa mwanga wa kutosha wa Jua hufanya mauwa kutokukuwa vyema na hatimae kuanguka.

7. Wadudu na magonjwa:
Uwepo wa baadhi ya wadudu wanaoshambulia mauwa na pia baadhi ya magonjwa ya fangasi kama botriytis na bacterial spot hupunguza nguvu ya mmea kuzalisha mauwa na matunda.

8. Sumu za wadudu na viuwa kuvu (sumu za ukungu/fangasi):
Baadhi ya sumu za wadudu zenye viambata vya Profenofos au imidacloprid au indoxacarb ni hatari zaidi kwenye Nyanya au hoho zilizo katika hatua ya mauwa.

Pia sumu za ukungu zenye metalaxy au hexaconazole, hazipendekezwi kupuliziwa kipindi cha mauwa, kwani zina athari katika ukomavu (stability) ya mauwa.

BONYEZA HAPA KUFAHAMU SUMU ZA MAGONJWA YA FANGASI AU KUVU AU UKUNGU.

USHAURI: Endapo utapulizia sumu zenye viambata tajwa hapo juu, Mkulima anashauriwa kufuatishia na booster ya mauwa ili kupunguza mshtuko uliosababishwa na ukali wa sumu za wadudu au fangasi (Kuvu).

KUEPUKA/KUPUNGUZA MAUWA KUPUKUTIKA/KUDONDOKA.

BONYEZA HAPA KUSOMA MAKALA YA KILIMO BORA CHA ZAO NYANYA.

1. Chaguwa aina nzuri ya mbegu yenye uwezo wa kustahimili mazingira ya Joto au baridi kulingana na mazingira eneo lako linapatikana; waweza kutupigia simu na kutuuliza kilimo for life .

2. Tumia kiwango sahihi na linganifu cha mbolea katika kila hatuwa; waweza kutupigia simu na kutuuliza kilimo for life kwa ushauri.

3. Mwagilia maji ya kutosha kipindi cha Joto kali

4. Dhibiti wadudu wasumbufu na magonjwa mbalimbali aina zote.

5. Tumia viuatilifu sahihi kwa wakati sahihi; waweza kutupigia simu na kutuuliza kilimo for life kwa ushauri.


NUNUA FORMULA ZA MBOLEA NA VIUATILIFU KWENYE KILIMO CHA NYANYA KWA MUONGOZO ZAIDI

WASILIANA NASI KWA MSAADA NA USHAURI KUHUSIANA NA KILIMO CHA MAZAO YOTE.

MBEGU BORA AINA ZOTE ZINAPATIKANA.

PIGA SIMU:
+255 757 139 423 Mr A Mpinga.

Baruwa pepe:
Kilimoforlife@gmail.com 

Instargram: kilimo for life 
Facebook: kilimo for life

BONYEZA HAPA UNGANA NA KILIMO FOR LIFE FARMERS WHATSAPP GROUP.

Maoni

Machapisho Maarufu