MUONGOZO MFUPI WA KILIMO CHA MAHARAGE



MUONGOZO MFUPI WA KILIMO CHA MAHARAGE


Na Mr. Mpinga +255 757 139 423


BONYEZA HAPA KUPATA FORMULA ZA KILIMO
Habari mpenzi msomaji na mfuatiliaji wa makala zetu, Hapa tutaelezea kwa ufupi kuhusiana na Kilimo cha maharage


Kilimo cha maharage ni rahisi na kinalipa sana kikifanyika kwa utaalamu na ufanisi. Gharama za kilimo cha maharage ni nafuu na ushindani wa zao sokoni sio mkubwa sana. 

NUNUA FORMULA YA KILIMO CHA MAHARAGE KUPATA MUONGOZO SAHIHI WA MBOLEA NA VIUATILIFU SHAMBANI 


Mkulima Hahitaji kusafiri, kinachofanyika ni kuwaita wateja waje shambani kwake na kuchukua mzigo.

Ekari moja ya maharage ya njano kwa maeneo mengi huvunwa gunia kati ya 8 – 12 kutegemea na matunzo shambani.

Shamba la maharage ukilima kwa kumwagilia unaweza lima mara tatu kwa mwaka . Hii ina maana ukilima ekari moja tu utakua na uhakika wa kipato cha uhakika  kila baada miezi 4.


UOTESHAJI WA MAHARAGE

MBEGU
Upandaji wa maharage ufanyike katika muda muafaka kutokana na eneo ili kuweza kupata maji ya kutosha (mvua) na wakati wa mavuno kunatakiwa kuwe na ukavu ili maharage yasiharibikie shambani.


AINA ZA MBEGU
Kuna aina nyingi za maharage ambazo zinaweza kupandwa kwa mfano (Rojo, Mshindi, Pesa, SUA 90 na Canadian wonder) ambazo ni mbegu zilizoboreshwa.


KIASI CHA MBEGU KWA EKARI
Kilo 15 hadi 20 za mbegu za maharage zinatosha kuotesha shamba la ekari moja shamba, 

UPANDAJI WA MBEGU

Namna ya upandaji wa mbegu za maharage
Inashauriwa kupanda maharage katika umbali wa  sentimita 50 (mstari kwa mstari) na sentimita 20 (mmea kwa mmea), panda mbegu mbili za maharage katika shimo moja, mbegu zinaweza kupandwa katika umbali wa sentimita 3 Chini ya Udongo.
 
MBOLEA 
Mimea ya maharage inahitaji virutubisho vya kutosha kutoka kwenye udongo ili kuweza kukua na kuzalisha matunda yenye afya.

 
Ni vizuri kutumia mbolea hai ambazo zinasaidia viumbe hai huweza kukua na kuendeleza kurutubisha udongo, kwa mfano mizizi ya maharage husaidiana na viumbe hai (nitrogen fixing bacteria) waishio kwenye udongo kutengeneza nitrogen. 

Nashauri Mkulima kutumia mbolea ya DAP Kuoteshea maharage: DAP yaweza tumika kipindi cha kusia mbegu au wiki 1 mara baada mche kuota.


UDHIBITI WA MAGUGU

Shamba lililokuwa safi dhidi ya magugu

Inashauriwa kupalilia shamba mara tu magugu yanapotokea na kabla mimea haijatoa maua. 

Palilia kwa jembe la mkono au kung'olea magugu na maotelea yote shambani, waweza tumia kemikali kudhibiti uotaji wa magugu kabla ya kupanda maharage shambani.

KUKABILIANA NA VISUMBUFU SHAMBANI 

 
 



Maharage hushambuliwa na wadudu na magonjwa mbalimbali. 

Miongoni mwa njia
za kuzuia, kukinga na kufukuza wadudu ni kuhakikisha kuwa mimea
ipo katika hali nzuri (imepaliliwa, nafasi ya kutosha na haijaharibika).

Pia kubadilisha aina ya mimea inayopandwa kwenye shamba moja mara
kwa mara husaidia kupunguza uwezekano wa wadudu kuongezeka.


KILIMO ANUAI (Organic Farming)
Kwa baadhi ya wadudu kama vile viwavi (African Ballworm) na magonjwa ya Fangasi huweza
kudhibitiwa kwa kutumia muarobaini au vitunguu saumu.

Maji ya muarobaini ni dawa nzuri sana kwaajili ya kufukuzia wadudu na kudhibiti magonjwa ya Fangasi na haina madhara yoyote kwa binadamu.

KEMIKALI: Tumia Viuatilifu kudhibiti magonjwa na wadudu wanaotokea shambani 


VIUWA DUDU MADHUBUTI
Duduba, dusuall, Duduwill, Wilcron, Cutter, Wiltigo, Liberate N.k 

VIUWA KUVU (MAGONJWA YA FANGASI): Innovex, buctril, ridomil, wilthane,Superwil, Folicur n.k



MAHARAGE KUKOMAA NA KUVUNWA.

Maharage yaliyokomaa na kukauka vizuri

Maharage ya kijani/ Mabichi yanatakiwa yavunwe kabla punje za maharage hazijakuwa sana. Hii ni kati ya wiki 7-8 baada ya kupanda. Maharage makavu huvunwa mara tu kiasi cha kuridhisha cha kukomaa na kukauka kinapokuwa kimefikiwa.

Asilimia 80 ya maharage yakishakomaa na kuanza kubadilika rangi (kukauka) au kwa aina nyingine kusinyaa yanakuwa tayari kwa mavuno.

Kwa kawaida mmea wote hung’olewa na kuwekwa juani ili uendelee kukauka kisha maharage hutolewa kutoka kwenye mmea na kuendelea kukaushwa ili kupunguza matatizo wakati wa kuhifadhi.

Baada ya kukauka hadi kufikia angalaua asilimia 12 ya unyevu, maharage yanatakiwa yahifadhiwe kwenye chombo chenye mfuniko kama vile ndoo ya plastiki au pipa na kuendelea kuyaangalia mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa wadudu hawajaingia na kisha kuyafunika tena.


MAVUNO KWA EKARI

Magunia ya maharage sokoni

Maharage yakihudumiwa vizuri zaidi shambani hutoa mavuno ya Gunia kati ya 10-15 kwa ekari Moja


SOKO LA MAHARAGE.

jitahidi kutafuta na kufahamu soko la maharage kabla ya Kuanza kilimo cha maharage, Soko la maharage hutofautiana kulingana na msimu.  Hivyo ni vyema Mkulima kufahamu soko lake kabla ya kuanzisha mradi.

Bei ya Gunia la maharage la kilo 120 huwa linauzwa sokoni kati ya 150,000/= hadi 200,000/= kutegemea  na msimu wa zao sokoni.


Wasiliana  nasi Kupata FOMULA itakayokuongoza ktk kila hatua ya upandaji, matumizi ya mbolea na viuatilifu shambani na utatuzi wa visumbufu Shambani

+255717 439 423 Mr Mpinga agronomist 

WASILIANA NAMI KWA MSAADA NA USHAURI KUHUSIANA NA KILIMO CHA MAZAO YOTE TANZANIA.


0757 139 423 Mr Mpinga

kilimoforlife@gmail.com

Maoni

  1. Habari kaka Mr Mpinga! Napenda kutoa shukrani zangu kwa muongozo mfupi ulioelezea, Mimi pia ni mkulima mdogo nipo Arusha. Ningependa ugusie zaidi kwenye masoko, hasa ya nje katika zao hili la maharage(Kama una ufahamu zaidi) maana najua ndiyo changamoto kubwa hasa kwa wakulima wadogo.

    JibuFuta
  2. Maharage hulimwa kwenye udongo wa aina gani

    JibuFuta
  3. Nice work and instructions. Tu nashukuru sana

    JibuFuta
  4. asante kwa elimu nzuri.
    ukanda wa kaskazin Moshi hasa maeneo ya MTPC n aina gani inafaa na wakati gani?
    na umeshauri tutumie mbolea hai, je tuichaj wakat wa kupanda au yakishaota?

    JibuFuta
  5. Very, labuda tu tunaomba mtuelekeze hata tarehe murua kwa upandaji wa maharage ya masika

    JibuFuta
  6. Very, labuda tu tunaomba mtuelekeze hata tarehe murua kwa upandaji wa maharage ya masika

    JibuFuta
  7. Very, labuda tu tunaomba mtuelekeze hata tarehe murua kwa upandaji wa maharage ya masika

    JibuFuta
  8. Habar kama mimi ni mkulima wa wa maharage napatikana mkoa wa kigoma nahitaji kujua ni mbolea gani naweza kuitumia kulingana na udongo unaopatikan kigoma

    JibuFuta
  9. Asante kwa somo zuri, nitakutafuta ili unielekeze zaidi

    JibuFuta
  10. Je, mborea inatakiwa itumike kiasi gani kwa heka moja? Na nidawa gani inafakutumia wakati wa maua ili kuupammea kupata maua kwa wingi?

    JibuFuta
    Majibu
    1. Tumia Mbolea Ya Matunda na Maua kama Easy grow FRUIT AND FLOWER

      Futa
  11. natamani kujua kuhusu sehemu ya ufafanuzi kuhusu soko la maharage licha yakuwa na na changamoto mbalimbali lakini makadirio yanaweza kutuhamasisha wasomaji hasa kuelekea kujikita kwenye ulimaji wa zao hilo kwa sababu all in all tuna hitaji pesa

    JibuFuta
  12. Natamani kujua nakupata elimu zaidi kufanikiwa katika kilimo cha nyanya

    JibuFuta
  13. Asante kwa muongozo wenye kuridhisha zaidi Mimi tatizo kubwa linalonikuta ni kwamba maharage Yana majani manne lakini yanakuwa ya njano Yale majani naweza tumia dawa gani ili yaweze kurudi katika hali yake ya kawaida

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho Maarufu