Mbegu bora ya tikiti

ANITA F1 


Na Mr. Mpinga
Habari mpendwa msomaji wa makala zangu za kilimo cha mazao mbalimbali kupitia mtandao wetu wa kilimo for life. 

Leo napenda nikujulishe uhalisia kuhusu KILIMO CHA TIKITI MAJI Aina ya ANITA F1 


ANITA F1 ni mbegu bora ya tikiti maji inayozalishwa na kampuni ya CONTINENTAL SEEDS COMPANY 
Ni mbegu jamii ya zebra (miraba) yenye ufanisi wa hali ya juu katika uzaaji matunda.


SIFA ZA ANITAF1 
Mkulima wa Tikiti Iringa akiifurahia na kustaajabu mavuno ya Anita F1 


  • hutoa matunda yenye uzito wa kilo 10-12
  • Huwahi zaidi kukomaa ndani ya siku 75-87
  • Anita F1 inastahimili saana magonjwa mengi
  • Inastahimili kanda zote za Afrika mashariki na mvuwa nyingi.
  • Haina tabia ya kupasuka mara baada ya kukomaa.
  • Tunda lake ni Tamu hadi nyama ya chini 
  • Nyama (flesh) ya tunda la apoorva F1 ni nyekundu 
  • Tunda la Anitq F1 lina mbegu ndogondogo kuliko matunda mengine.
Katika baadhi ya mikoa Anita F1 imekuwa ni chaguo la wakulima wote ambao wanapata kuishuhudia Anita F1 ikiwa shambani.

KIASI CHA MBEGU KWA EKARI.

Gram 500 (nusu kilo) pekee inatosha kupanda eneo la shamba la ekari moja 

NAFASI ZA KUPANDIA 

Panda mbegu moja moja katika kila shimo katika nafasi ya Sentimita 100 (mita 1) baina ya mashimo kwenye mstari na sentimita 200 (mita 2) baina ya mistari. 

MFUMO WA UMWAGILIAJI.

Mfumo mzuri zaidi wa umwagiliaji kwenye zao la tikiti ni Kulima na kutengeneza matuta na kupanda mbegu pembezoni mwa mifereji (furrow irrigation).

Matawi yakishakuwa na kurefuka huhamishiwa juu ya tuta na shina kubaki Pembezoni mwa mfereji wa maji.


UPANGAJI WA UZAZI 


NUNUA FORMULA YA KILIMO CHA TIKITI KUPATA MPANGILIO WA MBOLEA NA VIUATILIFU NA KUNENEPESHA MATUNDA
Baada ya matunda kuanza kutoka (fruit setting) unashauriwa kupunguzia idadi ya matunda katika Kila shina yabaki matunda 3.

Hii itasaidia shina kulisha virutubisho cha kutosha katika kila tunda kuhakikisha kila tunda linakuwa na afya na uzito mkubwa zaidi.

IDADI YA MATUNDA KWA EKARI 
Kwa mpangilio huo inakadiriwa kuwa: kwa ekari moja (4,900 M^2) 

Endapo utatumia nafasi ya Mita 2 kwa 1, kutakuwa na mashina 2,450 (plant population) kwa ekari 

Hivyo idadi ya matunda kwa ekari moja itakuwa ni 7,450.

Matunda haya ni yale yenye uzito wa kilo 8 hadi 12; endapo ulipunguzia idadi ya matunda katika Kila shina yabaki matunda 3.

KUMBUKA: Uzito wa matunda huendana zaidi na matumizi linganifu ya mbolea shambani.
Mr. Godfrey Mkulima kutoka Simanjiro aliponiletea zawadi ya tikiti la Anita F1 kama shukran 

Naomba nimalize kwa kuwasihi wakulima wafanye maamuzi magumu ya kilimo cha tikiti maji, 

Kwa mfumo wa soko la tikiti Tanzania: Anita F1 ni chaguo sahihi zaidi 

WASILIANA NAMI KWA USHAURI NA MSAADA WA MASUALA YA AGRONOMIA NA KILIMO BORA 

+255 757 139 423 MR MPINGA 
kilimoforlife@gmail.com 

Maoni

  1. Enter your comment...mkuu habari ya siku nyingi...kuna picha yako moja umeiambatanisha ktk maelezo ya kilimo cha tikiti...ya space ya 60cm shimo kwa shimo na 2mita mstari kwa mstari...na nimeipenda sana...KWA MINAJILI HIYO ITATOA MASHIMO 4060 ..JE NAHITAJI MBEGU KIASI GANI ZA APOORVA F1 ..ZA KUTOSHA MASHIMO 4060?NA BEI YAKE IKOJE KWA SASA? MAANA NATEGEMEA KULIMA MWEZI WA TISA TAREHE MOJA,NIKI SHAVUNA VITUNGUU...NATANGULIZA SHUKRANI

    JibuFuta
  2. Nmefurahi kupata elimu sahihi kutoka kwenye blog yenu hongeren San mpo vzur

    JibuFuta
  3. Safii...Hii ni nzuri na naipata zaidi. Swalii.. Efficiency ya dawa izo katika umaridadi wa iyo miche ni ipo

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho Maarufu