KILIMO BORA CHA TIKITI MAJI KWA MAVUNO FURAHISHI,Na Mr. Mpinga


MUONGOZO MFUPI WA KILIMO BORA CHA TIKITI MAJI KWA MAVUNO FURAHISHI


Image result for BEST WATER MELON HARVEST IN FARM


Na Mr Mpinga +255 757 139 423 
Kilimoforlife@gmail.com 

Mbegu bora za Tikiti maji: 

Anita F1,Sukari F1, Kito F1, Sugar queen F1, Shabiki F1 n.k (kilo 8-12) N.k

BONYEZA HAPA KUWASILIANA WHATSAPP

MFUMO BORA WA UMWAGILIAJI
Panda mbegu kwenye hizo alama nyeusi na pitisha maji katika mifereji iliyotengenisha matuta

ENDELEA...
MPANGILIO WA MBOLEA NA VIUATILIFU KATIKA ZAO LA TIKITI MAJI SHAMBANI

·         KUANDAA SHAMBA.
Tumia sumu ya Roundup kuuwa viotelea na majani yote kabla ya kulima au kupanda nyanya shambani.


·         WIKI 1-2 KABLA YA KUSIA MBEGU
Baaada ya kulima shamba, Pulizia Dawa ya kupalilia magugu ya stomper kuepusha uotaji wa magugu na viotelea aina zote shambani

·         WIKI YA 1 BAADA YA MICHE KUOTA
Mbolea: weka mbolea ya DAP, Yara mila winner, au Yaramila otesha 50 kg kwa ekari kuchochea ukuaji wa mizizi na ustawi wa zao shambani.

Kudhibiti magonjwa ya ukungu/barafu: pulizia sumu ya Ivory 72, Ebony 72, Linkmil 72 n.k kukinga au kutibu magonjwa yote ya ukungu/kuvu shambani kama vile ugonjwa wa kukauka, kata kiuno, bakajani wahi, bakajani chelewa, ubwiru chini, ubwiru unga.
Kumbuka: pulizia madawa ya ukungu kila baada ya wiki 1-2 kuepusha ueneaji wa magonjwa shambani.

Kudhibiti wadudu waharibifu: pulizia sumu ya dudumectin, wilcron au duduwill kudhibiti jamii zote za wadudu waharibifu, kama vile utitiri, vipepeo weupe, leaf minner, vimamba, minyoo wa ardhnini.k

SOMA: MUONGOZO KILIMO BORA CHA NYANYA

·         WIKI YA 3 BAADA YA MICHE KUOTA
Mbolea: weka mbolea ya kukuuzia kama vile NPK, Yara mila winner, UREA, n.k 50 kg/ekari ili kustawisha mmea Zaidi shambani.
Kumbuka kupiga dawa ya ukungu kila baaada ya wiki 1-2 na kupiga dawa ya wadudu waharibifu shambani kwa afya nzuri ya mmea.

·         MAUWA YAKIANZA KUSHAMIRI
Mbolea; weka mbolea ya yaraliva nitrabor au yaraliva calcinity 50 kg/ekari
Pulizia sumu ya super will, wilthane au wilzeb kutibu na kukinga magonjwa yote ya kuvu.

·         MATUNDA YAKISHA TOKA
Mbolea: weka mbolea ya yaraliva nitrabor chanaganya na NPK au  yaramila winner au CAN au UREA kujenga tunda lenye Afya, umbo kubwa, kuepusha tunda kuoza kitakoni na kuongeza maisha rufani baada ya tunda kuvunwa.


CONTINENTAL ANITA F1 
SHABIKI F1

Pulizia Ivory 72, Ebony 72, au Ridomil kukinga dhidi ya magonjwa ya kuvu kama vile ubwiru chini, ubwiru unga n.k
SOMA: MUONGOZO KILIMO CHA VITUNGUU MAJI

BONYEZA HAPA UNGANA NA KILIMO FOR LIFE FARMERS GROUP KWA MUONGOZO ZAIDI 

BONYEZA HAPA KUPATA MBEGU ORIGINAL KUTOKA KWA DISTRIBUTOR

MAWASILIANO:0757 139 423 Mr Mpinga; mtaalamu na mshauri wa kilimo.


Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho Maarufu