KILIMO BORA CHA VITUNGUU MAJI Na Mr. Mpinga


MUONGOZO WA KILIMO BORA CHA VITUNGUU MAJI KWA MAVUNO FURAHISHI.
Image result for large onion

Mbegu bora za vitunguu maji
·         SV 3070 F1, NEPTUNE F1, JAMBAR F1 n.k

MUONGOZO WA MATUMIZI BORA YA MBOLEA NA VIUATILIFU KATIKA ZAO LA KITUNGUU MAJI SHAMBANI

·         KUANDAA SHAMBA.
Tumia sumu ya max round au max round turbo kuuwa viotelea na majani yote kabla ya kulima au kupanda kitunguu shambani.



·         BAADA YA KUPANDIKIZA MICHE
Pulizia sumu ya wilstop siku 2-3 baada ya kupandikiza miche kuepusha uotaji wa magugu na viotelea aina zote shambani

·         WIKI YA 1-2 BAADA YA KUPANDIKIZA
Mbolea: weka mbolea ya DAP, Yara mila winner, au Yaramila otesha 50 kg kwa ekari kuchochea ukuaji wa mizizi na ustawi wa zao shambani
Kudhibiti magonjwa ya ukungu/barafu: pulizia sumu ya super will, wilthane au wilzeb kukinga au kutibu magonjwa yote ya ukungu/kuvu shambani kama vile kata kiuno, ubwiru chini, ubwiru unga.
Kumbuka: pulizia madawa ya ukungu kila baada ya wiki 1-2 kuepusha ueneaji wa magonjwa shambani.
Kudhibiti wadudu waharibifu: pulizia sumu ya dudumectin, wilcron au duduwill kudhibiti jamii yote ya wadudu waharibifu, kama vile utitiri, minyoo wa ardhini, mchwa n.k

SOMA: MUONGOZO MFUPI KILIMO BORA CHA TIKTI MAJI

·         WIKI YA 4-6 BAADA YA KUPANDIKIZA
Mbolea: weka mbolea ya kukuuzia kama vile NPK, Yara mila winner, UREA, n.k kustawisha kitunguu Zaidi shambani.
Kumbuka kupiga dawa za ukungu kila baaada ya wiki 1-2 na kupiga dawa ya wadudu waharibifu shambani kwa afya nzuri yammsea.

·         KITUNGUU KIKIANZA KUJENGA
Mbolea; weka mbolea ya yaraliva nitrabor au yaraliva calcinity
Pulizia sumu ya kuuwa wadudu ya wilcron, dudumectin au duduwill n.k kudhibiti minyoo wa ardhini na utitiri mwekundu na wadudu wengine waharibifu.

·         KITUNGUU KIKISHAJENGA
Mbolea: weka mbolea ya yaraliva nitrabor chanaganya na yaramila winner au CAN au UREA kujenga kitunguu chenye Afya, umbo kubwa na kuongeza maisha rufani baada ya kuvunwa.
Pulizia super will kukinga dhidi ya magonjwa ya kuvu kama vile ubwiru chini, ubwiru unga n.k

SOMA: MUONGOZO MFUPI KILIMO BORA CHA NYANYA

MAKALA HII FUPI NI KWA MUJIBU WA AGRONOMIST WA SEMINIS NA BIDDI AGROPRODUCTS ENTERPRISES LTD

BONYEZA HAPA UNGANA NA KILIMO FOR LIFE FARMERS GROUP KWA MUONGOZO ZAIDI SHAMBANI 

BONYEZA HAPA KWA MAHITAJI YA MBEGU AINA ZOTE 
MAWASILIANO: 0757 139 423 Mr. Mpinga: mtaalamu na mshauri wa kilimo 

Maoni

  1. habari Mr. Mpinga

    katika matumizi ya mbolea ni vipi nikiamua kutumia mbolea za samadi(Manure) katika shamba langu la vitunguu na kuachana na mbolea za viwandani, nini faida na hasara ju ya hili



    asante sana kwa kutuelimisha vema

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho Maarufu