KILIMO BORA CHA ZAO LA NYANYA
MUONGOZO WA KILIMO BORA CHA ZAO LA NYANYA KWA MAVUNO FURAHISHI
MPANGILIO WA MBOLEA NA VIUATILIFU KATIKA
ZAO LA NYANYA SHAMBANI
·
KUANDAA
SHAMBA.
Tumia sumu ya max round au max round turbo kuuwa viotelea na
majani yote kabla ya kulima au kupanda nyanya shambani.
·
BAADA YA
KUPANDIKIZA MICHE
Pulizia sumu ya wilstop siku 2-3 baada ya kupandikiza miche kuepusha
uotaji wa magugu na viotelea aina zote shambani
·
WIKI YA
1-2 BAADA YA KUPANDIKIZA
Mbolea: weka mbolea ya DAP,
Yara mila winner, au Yaramila otesha 50 kg kwa ekari kuchochea ukuaji wa mizizi
na ustawi wa zao shambani.
Kudhibiti magonjwa ya
ukungu/barafu: pulizia sumu ya super
will, wilthane au wilzeb kukinga au kutibu magonjwa yote ya ukungu/kuvu
shambani kama vile kata kiuno, bakajani wahi, bakajani chelewa, ubwiru chini, ubwiru
unga.
Kumbuka: pulizia madawa ya
ukungu kila baada ya wiki 1-2 kuepusha ueneaji wa magonjwa shambani.
Kudhibiti wadudu waharibifu: pulizia
sumu ya dudumectin, wilcron au duduwill
na wiltigo plus kudhibiti jamii yote ya wadudu waharibifu, kama vile KANITANGAZE, vipepeo weupe, leaf minner,
vimamba n.k
·
WIKI YA
3-4 BAADA YA KUPANDIKIZA
Mbolea: weka mbolea ya
kukuuzia kama vile NPK, Yara mila winner, UREA, n.k 50 kg/ekari ili kustawisha mmea
Zaidi shambani.
Kumbuka kupiga dawa ya ukungu
kila baaada ya wiki 1-2 na kupiga dawa ya wadudu waharibifu shambani kwa
afya nzuri ya mmea.
·
MAUWA
YAKIANZA KUSHAMIRI
Mbolea; weka mbolea ya
yaraliva nitrabor au yaraliva calcinity 50
kg/ekari
Pulizia sumu ya wiltigo plus
changanya na sumu ya wilcron, dudumectin
au duduwill kudhibiti KANITANGAZE na wadudu wengine wote waharibifu.
·
MATUNDA
YAKISHA TOKA
Mbolea: weka mbolea ya
yaraliva nitrabor chanaganya na NPK/ yaramila winner/CAN/ UREA kujenga nyanya
yenye Afya, umbo kubwa na kuongeza maisha rufani baada ya kuvunwa.
Pulizia super will kukinga dhidi
ya magonjwa ya kuvu kama vile ubwiru chini, ubwiru unga
SOMA: MUONGOZO MFUPI KILIMO CHA TIKITI MAJI
SOMA: MUONGOZO MFUPI KILIMO CHA TIKITI MAJI
MAWASILIANO: 0757 139 423 Mr Mpinga, mtaalamu na mshauri wa kilimo
MAKALA HII NI KWA MUJIBU WA AGRONOMIST WA SEMINIS NA BIDDI ENTEPRISES LTD. Mr. Mpinga
Naomba kitabu kiwe in PDF format
JibuFuta