KILIMO CHA BUTTERNUT MABOGA LISHE


Imeandaliwa na Abbas Mpinga
 +255757139423/717449423


Boga lishe (Squash butternut) ni zao jamii ya maboga (Cucurbit) ambalo hutumika zaidi kwa matunda ya shina lake. Ni moja ya zao lenye thamani na faida kubwa sokoni.
Shina la boga lishe huzalisha matunda jamii ya maboga yenye muonekano mfano wa vibuyu.
Maboga lishe huuzwa kwa uzito kuanzia kilo moja na wastani wa bei yake kwa mwaka 2020 na 2022 ni 1,000/= @kg 

Faida ya maboga lishe 
  • Ina virutubisho vingi vyenye faida kubwa mwilini 
  • Ni moja ya mazao ya biashara yenye faida kubwa 
  • Ina virutubisho vya carotene vyenye kuongeza afya ya macho 
  • Ina Vitamine A Yenye kuongeza Uzalishaji wa seli hai kuongeza kinga ya mwili na huongeza  uimara wa mifupa juu ya upatikanaji wa vitamin C.
Hali ya hewa: huota na kustawi vyema ktk wastani wa joto ridi la  18-25 °C.

Tindikali ya udongo: hustawi ktk hali ya udongo yenye tindikali ya wastani wa pH 6.0-6.5 

Kuandaa shamba.
Shamba kikwatuliwe vyema na kulainisha udongo kisha kunyanyulia matuta urefu wa futi moja ili kurahisisha upenyaji wa mizizi na kuzuia athari ya mvua.

Muda wa kupanda.
Boga lishe hupandwa muda wowote ispokuwa kipindi cha baridi kali huathiri ustawi wa mmea husika.

Kupanda.
Sia mbegu moja kwa moja shambani au unaweza kuandaa miche kwenye kitalu cha trei.

Kiasi cha mbegu 
500g (nusu kilo) za mbegu ya boga lishe hutosheleza kupanda ekari moja.

Nafasi.
Nafasi baina ya mistari ni mita 1 na nusu yaani sentimita 150 
Nafasi baina ya mashina ni sentimita 40.

Matumizi ya Mbolea
  • Wiki ya kwanza baada ya mbegu kuota: DAP 5g/shina 

  • Wiki ya 3 baada ya miche kuota: NPK 10g/shina 

  • Wiki ya 5 baada ya miche kuota: NPK 10g/shina 

Umwagiliaji 
Mfumo wa matone ni bora zaidi kwa kilimo hiki au mfumo usioruhusu majani kugusa maji.
Kiwango cha mm 25 hadi 40 kinatosheleza kumwagilia mche wa boga lishe kwa wiki nzima.


Kanuni za kiagronomia 
  • Kipindi cha baridi unaweza kutumia matandazo ya plastic (plastic mulches) au majani.
  • Kilimo cha mzunguko ni miaka 4
  • Punguzia magugu yakiwa machanga kwa kuyang’olea kwa mikono 
  • Nyuki hurutubisha maua na kutoa matunda, Hivyo nyuki wasiuliwe au kupigwa na dawa 
  • Zuia upepo mkali 
Mavuno 

  • Tumia kisu kukata tunda mwanzo wa kikonyo kutokea kwenye tawi.
  • Tumia mifuko safi kwajili ya kuvunia Maboga lishe.
  • Osha maboga lishe yenye udongo kabla ya kupeleka sokoni.

Mwisho.

Wasiliana nasi
+255757 139423 
+255717 439423 Abbas Mpinga 

kilimoforlife@gmail.com 


Maoni

Machapisho Maarufu