MUONGOZO MFUPI WA KILIMO BORA CHA ALIZETI


Imeandikwa na Abbas J. Mpinga 
+2557571(7174) 39423 
kilimoforlife@gmail.com 
Arusha Tanzania 


Alizeti ni moja ya zao la biashara linalotumika zaidi kwa kuzalisha bidhaa ya mafuta ya Alizeti. Mafuta ya alizeti ni moja ya mafuta ya kula yanayoaminika zaidi duniani kiafya.
Tanzania, Alizeti hulimwa zaidi Mikoa ya kanda ya kati, kaskazini, magharibi, mashariki na kanda ya ziwa.

Aina ya alizeti 
Kuna aina tatu ya alizeti duniani.

Oilseeds : aina hii hutumika kuzalisha mafuta ya kula 

Nonoilseeds: Aina hii hutumika kuzalisha chakula cha binadamu na mifugo, aina hii huwa na punje kubwa zaidi na haina mafuta mengi.

Conoil seeds: aina hii hutumika kuzalisha chakula cha binadamu na ndege 

Tanzania kuna aina tatu za mbegu za alizeti 
Mbegu za asili: hizi ni mbegu ambazo hulimwa na wakulima kisha mavuno hutenganishwa kwa mengine kuuzwa na mengine kuwekwa mbegu za msimu ujao.
Hizi hutoa gunia 2-3 kwa ekari; Mfano Tausi na Serena 

Mbegu zilizoboreshwa.
Hizi ni mbegu ambazo huzalishwa na mamlaka ya serikali wizara ya kilimo  na tasisi zake Za mbegu (ASA) na makampuni binafsi.
Huwa na uwezo wa kuzalisha zaidi ya gunia 5 kwa ekari moja: Mfano Record 

Mbegu chotara 
Hizi ni mbegu zinazozalishwa na makampuni binafsi nje ya nchi na kukubaliwa kuingizwa nchini na mamlaka ya udhibiti ubora wa mbegu na vipando nchini TOSCI
Hizi huzalisha zaidi ya gunia 8-10 kwa ekari. Mfano HYSUN, SUPERSUN, JAGUAR n.k

Hali ya hewa: jotoridi la wastani wa 18 hadi 28 °C ni afuani kwa Kilimo cha alizeti 

Udongo: udongo wenye rutuba, unaopitisha na kuhifadhi maji muda mrefu.
tindikali ya udongo ni pH 6.5-7.5

KULIMA 
Alizeti hulimwa kwa shamba la sesa au matuta, hivyo shamba liandaliwe mapema kwa kukwatuliwa vizuri na kusawazisha udongo kabla ya kusia mbegu 

Kiasi cha mbegu:
Kilo 2 - 3 hutosheleza kupanda ekari 1

Kiasi cha mimea shambani 
Shamba la ekari moja linapaswa kuwa na mshina 25,000 hadi 30,000 ya alizeti 

Nafasi baina ya mashina 
Aina ndefu inapaswa kuachanishwa kwa sentimita 60 baina ya mistari na 30 baina ya mashina.

Aina fupi inapaswa kuachanishwa kwa sentimita 45 baina ya mistari na 30 baina ya mashina.

Sia mbegu kina cha sentimita 2-3.

Siku 12 baada ya alizeti kuota, alizeti zilizobanana zinapaswa kung’olewa ili kuachananisha nafasi kwa sentimita 30 baina ya alizeti ktk mistari 

Kupalilia 
Shamba la alizeti linahitaji Palizi ya haraka kwani magugu mengi ni hatari kwa uzalishaji wa alizeti.
Waweza tumia viuagugu vya kudhibiti uotaji wa magugu kabla ya kusia alizeti au baada ya alizeti kuota na kabla magugu hayajaota. Mfano Alazine, Atrazine, pendamethalimi n.k

Mbolea 
Tani 12 hadi 15 za samadi kwa ekari kwenye shamba lisilo na rutba  kila baada ya miaka 2 hutosheleza saana kwa virutubisho kwenye mmea wa alizeti shambani.

Kwa shamba lisilo na rutuba, waweza weka mbolea ya DAP siku 12 tangu kuota/baada ya kung’olea 

Pia weka NPK 17:17:17 Siku 30 tangu alizeti kuota

Waweza pulizia mbolea ya maji Yaravita boost siku 25 baada ya alizeti kuota.

Umwagiliaji
Alizeti hulimwa zaidi kipindi cha mvua na kwa uchache hulimwa kwa kumwagilia.
Hakikisha alizeti inapata maji vizuri kipindi cha baada ya kuota na kipindi cha kujaza mbegu (grain filling) hivyo ni vipindi muhimu zaidi vya umwagiliaji.
Mwagilia alizeti mara baada ya unyevu kukauka ardhini.

Magonjwa na wadudu
Dhibiti wadudu waharibifu kwa kuwapulizia viuadudu imara mapema kabla hawajaleta madhara makubwa.
Magonjwa ya alizeti ni mengi na hususani zaidi ni ubwiri unga, dhibiti ugonjwa huu kwa kupulizia kiuakuvu chenye kiambata cha  metalaxy au carbendazim au dimethomorph au Ozystrobin n.k 
Wasiliana nasi kwa ushauri zaidi.

Kudhibiti Ndege

Ndege ni hatari zaidi kwenye kilimo cha alizeti kwani wasipodhibitiwa husababisha hasara ya zaidi ya Asilimia 45 hadi 90.
  • Dhibiti ndege kwa kulinda shamba lako nyakati za mchana.
  • Funika vichwa vya alizeti kwa nailoni nyeupe.
  • Tumia Dawa zenye harafu mbaya kwa ndege kupulizia shamba zima.
  • Tumia kadi zenye Mng’ao kudhibiti ndege, Wasiliana nasi kupata kadi hizo.
Kuvuna 
Alizeti huwa tayari kuvunwa endapo kiwango cha unyevu cha mbegu za alizeti kitafikia 20% m.c au chini ya hapo.
Alizeti huwa tayari kwa kuvunwa mara kichwa cha alizeti kibadilika rangi na kuwa njano hadi kahawia.
Vichwa vya alizeti vikishavunwa vikaushwe juani vizuri kisha vipigwepigwe kwa kutumia vijiti au machine (thresher).

Alizeti ikihudumiwa vizuri shambani huzalisha zaidi ya gunia 8-10 kwa ekari moja.

Kuhifadhi.
Hifadhi alizeti kwenye magunia safi baada ya kukauka vizuri juani kuepuka kuharibika ghalani.

Masoko.
  • Soko la alizeti ni rahisi zaidi;
  •  waweza uza alizeti kama malighafi
  •  waweza kamua alizeti na kuuza mafuta
  •  waweza kamua alizeti na ukauza mafuta pamoja na mabaki (mashudu)
Imeandikwa na Abbas J. Mpinga Agronomist 
+2557571(7174) 39423 
kilimoforlife@gmail.com 
Tanzania 





Maoni

  1. Hongera sana kka. Naomba kujua what if hizo aina tukaziandika kwa kiswahili kwa pembeni..!Will it sound good?
    All in all keep moving my bro..πŸ’ͺ

    JibuFuta
    Majibu
    1. Nimetafuta maana ya kiswahili sijaona na aina zingine hazipatikani saana east africa

      Futa
  2. Hongera Sana bro. I appreciate the work of youth

    JibuFuta
  3. PowerfulπŸ‘ŠπŸ»πŸ‘ŠπŸ»πŸ‘ŠπŸ»

    JibuFuta
  4. Congratulations Mr. Abbas,
    This is super πŸ’ͺπŸ’ͺ

    JibuFuta
  5. Nice bro....it has been helpful.

    JibuFuta
  6. Wadudu gani ni waharibifu wakati na kabla mbegu ya alizeti kuota??

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho Maarufu