UGONJWA WA BAKAJANI CHELEWA KWENYE NYANYA (LATE BLIGHT)

 UGONJWA WA BAKAJANI CHELEWA KWENYE NYANYA (LATE BLIGHT)

Na Mr. Mpinga agronomist 

☎️+255757 139423

📞+255717 439423

BOFYA HAPA KUPATA FORMULA ZA KILIMO

📧abbas.mpinga@continentalseeds.com 


📧Kilimoforlife@gmail.com 


Nasikitika kusema kuwa ugonjwa wa bakajani chelewa (late blight) unaosababishwa na Vimelea kuvu _(Phythopthora infestans)_ kwenye nyanya ni ugonjwa hatari zaidi kuliko magonjwa yote kwenye zao hili.


Ugonjwa wa bakajani chelewa huenea zaidi kipindi cha mvua na hali ya ukungu au unyevu wa muda mrefu.


Ni ugonjwa mgumu kudhibitika mara utokeapo. 


DALILI

Hali ya majani kuwa na madoa ya kuungua ungua na tunda la nyanya kuwa na hali ya weusi wa kuoza maji kwa ndani.


Ugonjwa huu baada ya masaa 48 bila kudhibitiwa,  Shamba zima huwa na hali ya kuungua kabisa bila ya majani kupukutika.


KUDHIBITI 

Ugonjwa huu ni mgumu kudhibitika kirahisi mara ueneapo.



Tumia copper oxychloride au mancozeb kukinga kila baada ya siku 7 kipindi cha mvua nyingi au ukungu na unyevu mwingi.


Endapo mvua itanyesha muda mfupi baada ya kupulizia kiua kuvu,  Unashauriwa kurudia mara hali itapo kaa shwari.


Endapo dalili zitaonekana mapema: Tumia kiua kuvu chenye kiambata cha Oxystrobin kama vile Biddistar n.k kutibu ugonjwa kabla haujakomaa ikiambatana na kutoa majani na matunda yaliyoanza kuathirika.


Endapo ugonjwa utakuwa umeenea,  Unashuriwa kusafisha shamba mapema. 


Tembelea blog yetu kujifunza zaidi 


www.kilimoforlifetz.blogspot.com

https://www.instagram.com/p/COdCSxBna_-3G2REw4bvEvRuINopjPuPBrSCdA0/?igshid=1tf034ceozc3j


Maoni

Machapisho Maarufu