POTASSIUM NUTRIENT (K) (KIRUTUBISHO CHA POTASHIUM)

Na Mr. Mpinga agronomist 

+255757 139 423

+255717 439 423

abbas.mpinga@continentalseeds.com 

Kilimoforlife@gmail.com 

BOFYA HAPA KUPATA FORMULA ZA KILIMO

Potassium (K) ni Moja ya virutubisho muhimu sana kwenye mazao ya mbogamboga yazalishayo Matunda (fruiting vegetables) kama vile Nyanya,  Pilipili, biringanya, n.k 

Potassium husaidia mmea kuimarisha usambazaji maji ktk mwili wa mmea,  uchakataji wa chakula (sukari), ushamirifu wa maua na uimara wa matunda.

Potassium hupatikana ktk mbolea ya NPK, MOP, Yaramila, Otesha,  yaramila winner, mbolea za Maji kama vile Mult K, n.k 

kiwango kikubwa cha K katika ardhi ya chumvi husaidia kuimarisha ukuaji wa mmea kwa muda wote shambani 

Potassium husaidia mmea kushamirisha mauwa mengi 

Potassium husaidia mmea kuzalisha matunda mazuri yenye kiwango linganifu cha sukari, kuiva vizuri na maisha rufani (life span)

UPUNGUFU WA POTASSIUM 

Upungufu wa Potassium husababishwa zaidi na Tindikali ya udongo (Soil pH) kuwa kubwa sana au ndogo saaana.

Tindikali rafiki kwa Potassium ni ya wastani wa 6.0 - 6.5 juu ya 5.8 chini ya 6.8.

husababisha uivaji hafifu wa matunda (Blotchy ripening)

Tishu za ndani ya shina kubadilika rangi na kuwa nyeupe 

Majani kubadilika rangi kutokea pembeni na kuelekea kwenye umanjano 

Kiwango kingi cha Potassium huongeza Tindikali kwenye Tunda la nyanya na hivyo kuepusha kuoza haraka 

Kiwango kikubwa cha Potassium pia huathiri upatikanaji wa madini ya calcium na magnesium kwenye mmea.

Kiwango kingi cha madini ya Sodium huathiri upatikanaji wa K kwenye mmea.

KUMBUKA: Tumia mbolea za majani (foliar fertilizer) zenye K  endapo udongo hautokuwa rafiki kwa upatikanaji wa kirutubisho K.

MATUMIZI YA K KWENYE MAZAO YA MATUNDA 

1. Kipindi cha kuanzia: kuchochea ukuaji wa mmea kwa hatua ya mwanzo 

2. Kipindi cha kukuuzia: kuchochea ukuaji wa sehemu zote za tishu za mmea kuandaa mmea kwaajili ya maua 

3. Kipindi cha maua: kustahimilisha na kuhimilisha ukuaji wa mmea na kuchochea uzalishaji na ushamirifu wa maua 

4. Kipindi cha matunda: kukuza, kukomaza na kuivisha matunda pia kupunguza mapungufu ya matunda (Fruit disorders).

Kiwango kikubwa cha K kinahitajika hatua ya 3 na 4

Inaendelea.........

Tembelea blog kujifunza zaidi 

www.kilimoforlifetz.blogspot.com 

#kilimoexpert 

#kilimoforlife 


Wasiliana nami kupata FOMULA za mpangilio wa matumizi ya mbolea na viuatilifu ktk mazao mbalimbali 


+255757 139 423

+255717 439 423

Maoni

Machapisho Maarufu