FAIDA YA KULOWEKA MBEGU KABLA YA KUSIA (PRE-GERMINATION)

 FAIDA YA KULOWEKA MBEGU KABLA YA KUSIA (PRE-GERMINATION)


Kitendo cha kuloweka mbegu kabla ya kusia shambani ni kitendo cha kitaalamu kijulikanacho kama Pre-germination. 

Wakulima wengi husumbuka kutokana na tatizo la mbegu kutokuota vizuri (Poor germination %) au kuchelewa kuota (Late sprouts). Hii hutokana na matatizo ya kimazingira,  mbegu au namna ya uoteshaji. Ni vyema kuloweka mbegu kabla ya kusia ili kunufaika na miongoni mwa faida za kuloweka mbegu kabla ya kusia. 

Mbegu hulowekwa ndani ya maji vuguvugu (sio maji moto) kwa masaa kadhaa ili kulainisha ganda la mbegu (seed coat) na kuifanya mbegu kunywa maji kwa haraka na kusaidia kuota haraka zaidi ipelekwapo shambani.

Mbegu huota haraka kwa muda mfupi zaidi kuliko ingepandwa bila kulowekwa 

Asilimia za uoataji wa mbegu (Germination percentages) huongezeka  kuliko mbegu ingepandwa bila kulowekwa 

Husaidia kupunguza muda wa miche kukaa kitaluni hivyo kukomaa haraka kabla ya kupandikizwa 

NAMNA YA KULOWEKA MBEGU 

Chukua maji safi kisha chemsha kupata uvuguvugu kuua bacteria na vimelea hatarishi.

Haifai kutumia maji ya moto sana kwani yanaweza kuunguza mbegu 

Loweka mbegu kwenye chombo safi kilichofunikwa vizuri kwa muda wa saa 12 na usiozidi saa 48.

Maji yanapokuwa na uvuguvugu mkubwa ndivyo muda wa kulowekwa mbegu hupungua 

Baada ya kuloweka mbegu hakikisha mbegu imevimba na imelainika vizuri kabla ya kusia 

Usiruhusu mbegu ikauke kabla ya kusia 

Hakikisha baada ya kusia mbegu unafuatisha na kumwagilia maji ya kutosha shambani kutoruhusu mbegu kuoza. 

Sio kila mbegu inanufaika na ulowekaji,  baadhi ya mbegu kama karoti,  nyanya,    n.k hazinufaiki kukubwa kutokana na ulowekaji.

Mbegu zinazonufaika na ulowekaji ni kama mahindi, Maboga,  tikiti,  alizeti,  maharage,  kabeji,  zucchini,  na mazao jamii ya yaliyotajwa hapo juu. 


IMEANDALIWA na 

Mr Mpinga agronomist 

📞+255757 139 423

✉️ abbas.mpinga@continentalseeds.com 

📩kilimoforlife@gmail.com

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho Maarufu