Tatizo la nyanya, hoho na tikiti kuoza kitako, Blossom endrot
LIJUE TATIZO LA KUOZA KWA MATUNDA KWENYE KITAKO (BLOMSOM END ROT)
BONYEZA HAPA KUPATA FORMULA ZA KILIMO
Blossom End Rot (makovu meusi kwenye kitako cha tunda Hii ni changamoto inayotokea san katika Mazao Kama Nyanya, Tikiti, Bilinganya, Tango na mengine. Kitaalam huu sio ugonjwa bali ni tatizo .Tatizo hili hutokana na upungufu wa madini ya Calcium na /au umwagiliaji usiokuwa na mpangilio.
Huu sio ugonjwa wala wala madhara yatokanayo na uharibifu wa wadudu, ni ulemavu wa kiumbo unaotokana na upungufu wa Calcium katika tunda.
Chanzo kikuu cha tatizo hili ni umwagiliaji usiokuwa na mpangilio. Ukosefu wa maji ya kutosha husababisha upungufu au kiwango cha Calcium katika mmea. Ufyonzwaji wa Calcium kwenye mimea unauhusiano wa moja kwa moja na upatikanaji wa maji ya kutosha.
Nutrient Imbalance (Kutokuwepo Usawa wa Virutubisho)
Excess potash(Kuzidi kiwango cha Potassium kwenye udongo)
Inapotokea kiwango cha kirutubisho cha Potassium kimezidi au kipo kwa wingi kwenye udongo, hupunguza au kuzuia ufyonzwaji wa madini ya Calcium na hivyo kusababisha tatizo hilo.Kiwango cha Potassim kinaweza kuzidi hasa pale mtu anapotumia mbolea zenye potassium kwa kiwango kikubwa kuliko inavyoshauriwa kwa zao husika.(Recommended amount).
Jinsi ya kuzuia Tatizo.
Umwagiliaji
Kitu cha msingi kabisa ni kuhakikisha udongo wako au ardhi yako inakuwa na unyevu au haikauki na kubaki kavu kabisa. Hakikisha kuna unyevu kwa ardhi yako japo kwa mbali na usiruhusu kabisa ardhi kuwa kavu .Ukame ni kitu kingine kinaweza kusababisha tatizo hilo ndio Maana kipindi Cha kiangazi tatizo ni kubwa zaidi.
Matumizi ya Mbolea
Kama umeshauriwa kutumia mbolea zenye potassium ktk lako, hakikisha hutumii kiwango zaidi ya kile ulichoshauriwa.Kama umeshauliwa kutumia gram tano weka ,gram tano.Kama ni kumi tumia kumi.Potassium ikizidi,inakwenda kuzuia kabisa ufyonzwaji wa Calcium.Ikiwa Hali hii itazidi Basi Calcium itashindwa kufyonzwa ipasavyo na hivyo kusababisha tatizo hilo.
KUZUIA TATIZO (Bloomsom End Rot).
Hakuna tiba ya tatizo hilo kama tunda limeshaathirika. Mapema tu unapogundua tunda lina tatizo hilo,liondoe kutoka kwenye mmea husika. Ni vizuri na salama zaidi kulichimbia chini na kulizika kabisa. Hii husaidia nguvu na chakula nyingine/kingine kuelekea kwenye matunda ambayo hayajaathirika na hatimae kupata matunda mazuri zaidi.
Weka mpangilio au ratiba nzuri ya Umwagiliaji kuwe na muda maalumu wa kumwagilia. Hii itasaidia kutatua tatizo katika njia mbalimbali. Kama matunda yataendelea kuathirika licha ya kuwa na ratiba nzuri ya kumwagilia, unahitaji kuangalia kiwango cha Calcium na Potassium na kufanya utaalamu wa kurekebisha kiwango kiwe sawa.
Kuongeza kiwango cha Calcium katika mmea, unaweza kunyunyiza mbolea za maji zenye Calcium Nitrate angalau mara tatu kwa wiki kwa muda wa wiki mbili na badilisha kwa mlisho wa kawaida kwa kumwagilia mara moja kwa wiki maji yaliyochanganywa na mbolea ya Calcium Nitrate.
JINSI YA KUCHANGANYA MBOLEA KUDHIBITI TATIZO
Calcium Nitrate Kama mbolea ya Majani.
Changanya kijiko kimojaa kisijae sana(1 level table spoon of Calcium Nitrate ) katika lita moja ya maji na mwagiia kwenye majani kama unavyofanya kwa viuatilifu zlvya kawaida na mbolea za majani.
Calcium Nitrate Kama mbolea ya kupiga kwenye Udongo.
Changanya kiwango kama kiichoelekezwa hapo juu, na kisha piga kwenye mashina kama mtu anamwagilia.
Pia mkulima anaweza kutumia Mbolea nyingine zinazoweza kutoa Calcium kwa haraka kama Yaraliva Nitrabor/Calcibor/ Calmax/ Omex, ili kunusuru hali hiyo.Zipo mbolea nyingi zinazoweza kutumika kudhibiti tatizo hilo, na zilizotajwa hapo ni mfano tu.
BONYEZA HAPA KUPATA FOMULA ZA MBOLEA
Imetayarishwa na:
Eliya Joseph Kituye.
Technical Field and Sales Agronomist.
Bytrade Tanzania Limited.
Dar-Es-Salaam-Tanzania
Imehaririwa na kuchapishwa na
Mr Mpinga CEO KILIMO FOR LIFE
Agronomist and sales representative
CONTINENTAL SEEDS COMPANY LTD.
TANZANIA
+255 (7571) (7174) 39423
kilimoforlife@gmail.com
TUNAUZA FORMULAR ZA MATUMIZI YA MBOLEA NA VIUATILIFU KWENYE MAZAO YOTE KWA GHARAMA NAFUU
TUNATOA USHAURI NA MIONGOZO YA KILIMO BORA (CONSULTATIONS) NA TUNASIMAMIA MASHAMBA MAKUBWA KWA MIKATABA NAFUU SANA. WASILIANA
Maoni
Chapisha Maoni