NAMNA YA KUHIFADHI VITUNGUU MAJI
Namna ya kuhifadhi kitunguu maji kwa muda mrefu niliyojifunza kwa mkulima
1. Chimba shimo lenye kina cha foot kadhaa Kwenda chini.
2. Juu yake jengea kichanja chenye ngazi usawa wa mita 1 kutoka chini, na ngazi (floor za vichanja) zitenganishwe na wiremash.
3. Juu ya kichanja funika kwa paa imara mfano bati lenye pembe ndefu kutokuruhusu unyevu kuingia ndani.
4. Tafuta maranda ya mbao na mwaga ktk shimo usawa wa futi moja.
5. Fuatiliza na Changarawe kwa juu usawa wa nusu futi kisha weka samadi mbichi iliyokauka juu ya changarawe.
6. Hifadhi vitunguu ktk magunia mazito na cyo ya sandarusi/neti.
7. Laza magunia juu ya kichanga, kuanzia ngazi za chini kwenda ngazi za juu (bed floors).
8. Choma maranda kila asubuhi na yaunguwe hadi jioni kisha jioni zima moto.
9. Fanya hivyo mpaka maranda yatapoisha na kitunguu kitakuwa tayari kuhifadhika muda mrefu takribani miezi 8 hadi 12.
10. Nitaleta mchoro wa picha na maelezo ya namna ya kuwasha na kuzima.
Ahsanteni sana
By Mr Mpinga agronomist
BONYEZA HAPA KUWASILIANA WHATSAPP
+255757139423/717439423
KWA MAHITAJI YA MBEGU BORA ZOTE WASILIANA NAMI
Maoni
Chapisha Maoni