NAMNA YA KUANDAA KITALU BORA; preparation of nursery soil
NAMNA YA KUANDAA KITALU CHA MAZAO YA MBOGAMBOGA
Na Mr Abbas Mpinga: +25571739423/255757139423
BONYEZA HAPA KUPATA FOMULA ZA MBOLEA KWENYE MAZAO
MAHITAJIO
1. Udongo pori (forest soil): udongo wajuu unaopatikana msituni au chini ya mti mkubwa.
Chimba udongo wa juu (mweusi wenye rutuba) bila kuchanganya na udongo wa chini
2. Samadi iliyowivu vizuri muda wa miaka miwili hadi mitatu
3. Pumba za mpunga au maranda ya mbao au mchanga halisi kabisa.
Chaza (Sanitize) udongo pori katika moto kwa kutumia pipa au karai chuma kisha funga (pipa au karai) kutokuruhusu moshi kutoka nje.
Changanya udongo ndani ya pipa au karai CHUMA kila baada ya dakika 10 kuruhusu moshi kuchanza udongo wote.
Zima moto udongo unapofikia joto la sentigrade 70⁰ C.
Changanya Udongo pori : Samadi : Pumba/maranda/mchanga kwa uwiano wa 4:2:2
Mfano
Ndoo 4 za Udongo: ndoo 2 za Samadi: Ndoo 2 za Pumba au maranda au mchanga.
Changanya vizuri kisha mwaga mchanganyiko huo ktk sehemu ya wazi au trei za kuoteshea miche ambapo mbegu zitaoteshwa rasmi.
Kitalu Kiwe na Ukubwa wa mita 4 za mraba.
Funika kitalu kwa nailoni nyeusi au majani mengi kuongeza joto kwenye udongo ili kusaidia mbegu kuota haraka.
Baada ya mbegu kuota funua na weka nailoni au neti nyeupe kwa juu au pandisha majani na yawekwe juu kwa mfumo wa kichanja.
Siku 7 hadi 10 kabla ya kuhamisha miche (kutuliza) shambani, Ondoa nailoni au kichanja kuruhusu miche kupigwa na jua ili kuizoesha mazingira mengine ya shambani kabla ya kuhamishwa rasmi.
MWISHO
Wasiliana nami
+255757 139 423
+255717 439 423 Mr Abbas Mpinga
MBEGU AINA ZOTE ZINAPATIKANA KWA BEI NAFUU
www.kilimoforlifetz.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni