Jifunze kutoka kwa mkulima mkubwa kutoka Arusha
BONYEZA HAPA KUWASILIANA WHATSAPP
Mnamo saa 10 ya alaasiri nikiwa naandika report ya kazi, nilimpigia simu mkulima wangu anaejulikana kwa jina la Mr Alex, Mchaga wa marangu ili kumuuliza maendeleo ya
shamba la majaribio kwa mbegu nilizompatia
Mr Alex aliniomba nimtembelee ili nione kwa macho yangu kile kinachoendelea na huwenda ningeweza kumshauri zaidi kwa chochote ambacho ningekiona.
Kwasababu hakuwa mbali sana na pahala nilipokuwa, niliahirisha kazi yangu na kuanza safari fupi kuelekea Sombetini- Dispensary
Baada ya kufika nilijionea maendeleo ya shamba la Mr Alex pia akajivunia vile anapiga pesa nyingi kwa kuuza nyanya ya Ranger F1 ambayo ni imezaa saana tofauti na alivyotegemea.
Mr Alex alinishangaza kwa kuwa ni miongoni mwa wakulima wachache wenye miradi mingi zaidi kuwahi kuwatembelea: Ana mabwawa mawili makubwa ya samaki, Ana boma kubwa la ng'ombe, Ana shamba la kuku, Mbuzi na mashamba ya mazao zaidi ya ekari 100.
Nilifurahishwa vile anavyozungumza na ng'ombe wake mithili ya binadamu wenzake, kwani amewataja ng'ombe wake kwa majina tofauti tofauti, mfano tengeru na sun white.. Ni raha sana kushuhudia
*Nilipomuuliza siri ya mafanikio yake Mr Alex alinijibu kuwa: siri ya mafanikio yake ipo chini ya wazazi wake*
Alinambia amejitahidi kufanya wazazi wake wawe na furaha juu yake muda wote na ndiyo anahisi kuwa yale aliyonayo ni rejea ya baraka za wazazi wake..!
Alinambia kuwa watu wengi hawanufaiki na utajiri wao kutokana na visirani vya wazazi wao kwao, mwisho wa siku wanafilisika ama kujitumbukiza kwenye ulevi na mambo mengine ya anasa zisizo na tija!
Mr Alex alisisitiza saana kuwa mtu asiwatenge wazazi wake kwa yale aliyofanyiwa kwayo; Bi maana hata kama wazazi walikutelekeza ama kukufanyia mabaya yeyote, bali mtoto kama mtoto jitahidi kuwa ni furaha ya wazazi wako!
Maneno yale yalinisisimua sio moyo wangu tu, bali hadi ngozi yangu, kwani ni maneno mazito ambayo sikutaraji kuyapokea kutoka kwa mtu kama yule ambaye ukikutana nae mjini, muonekano wake hauakisi Thamani yake!!
Kweli waswahili walisema......"Tembea uyaone"
Pia Mr Alex, akajivunia sana yeye kuwa na watoto wengi (12) na wote anawafundisha shughuli za kujitegemea, zile anazofanya yeye!!
Mwisho Mr Alex alinipatia Lita 1 ya maziwa na mboga mboga aina ya saladi!!!
Nilimshukuru saana, kisha nikaanza safari fupi ya kurejea kwangu, na mara baada ya kurejea Mr alex kwa kuwa ni mtu wa aina yake, alinipigia simu kuhakikisha kama nilifika salama!
KUNA FUNZO KUBWA SANA KUTOKA KWA MR ALEX KATIKA SAFARI YETU YA MAFANIKIO
Heko heko Mr Alex
Visit
Website: www.kilimoforlife.com
Instagram: Mr Mpinga
Twitter: Abbas Mpinga
Facebook: Abbas Mpinga

Ranger F1 |

Maoni
Chapisha Maoni