TATHMINI FUPI YA GHARAMA ZA KILIMO CHA NYANYA

TATHMINI FUPI YA GHARAMA ZA KILIMO CHA NYANYA
Mr. Mpinga Agronomist 



KILIMO FOR LIFE ni moja ya mtandao wa kilimo unaoongoza kwa kusomwa na kupitiwa na wasomaji na waperuzi wengi zaidi.
Ni mtandao ulioanzishwa na
Mr A. Mpinga mwenye nia,dhamira na malengo ya kumsaidia Mkulima kunufaika na fursa ya kilimo kwa kumuwezesha kufahamu mbinu na namna bora zaidi ya kukiendea kilimo cha kitaalamu kwa kufuata Kanuni bora zaidi za Agronomia na Matumizi sahihi ya mbolea na viuatilifu pia kutoa tathmini ya gharama za kilimo cha mazao mbalimbali.

Hapa tutaainisha  kwa ufupi kuhusiana na tathmini ya gharama kilimo cha nyanya.
Wakulima wengi nchini wamekuwa wakisumbuka saana huhusiana na Jambo hili. Na mara nyingi tumekuwa tukipigiwa simu kuulizwa kuhusiana na jambo hili.

Ikumbukwe kuwa: kutokana na kutofautiana kwa baadhi ya gharama kulingana na ukanda, Tumeweka wastani wa gharama za Mbolea, Na viutilifu.

KUMBUKA: KILIMO FOR LIFE TUNA KILA AINA YA MBEGU

KARIBUNI
Imeandaliwa na Mr Mpinga +255 757 139 423.
Facebook: kilimo for life 
Instagram: kilimo for life 
Email: kilimoforlife@gmail.com 

BONYEZA HAPA KUFAHAMU MBEGU BORA ZA NYANYA

 GHARAMA ZA MBOLEA KILIMO CHA NYANYA

Gharama ya Mbolea hutofautiana kulingana na ukanda!

mbolea ya kuanzia (wiki 1 -2 baada ya kupandikiza)

YARA MILA OTESHA au DAP 50 KG- 67,000-69,000 /=
Matumizi: Gram 5 kwa kila shina

Mbolea ya kukuuzia (wiki 2-3 baada ya kupandikiza)
YARA MILA WINNER au NPK 50 Kg- 69,000 -90,000/=
Matumizi: Gram 8 kwa kila shina

MBOLEA YA MAUWA (wiki ya 4 baada ya kupandikiza)
YARA Liva Nitrabor au Yaraliva Calcinity 50 Kg- 76,000- 80,000/=
Matumizi: Gram 8 kwa kila shina

Mbolea ya mauwa na matunda (wiki ya 5)
Changanya kwa ujazo wa uwiano sawa mbolea ya
 YARA Liva Nitrabo 50 Kg + Yaramila winner 50 KG = 69,000-90,000/= + 76,000-80,000/=
Matumizi: Gram 8 kwa kila shina

Baada ya michumo kuendelea utakuwa unaweka yaramila winner + yaramila Nitrabor kuchochea mavuno zaidi  na afya bora ya mmea

SUMU ZA WADUDU

Dudumectin,Snowthurder,Snowmectin au Duduacelamectin 1L- 25,000 -30,000/=

Matumizi: 30mls/20 L za maji

Utapulizia mara baada ya kuona wadudu ( lita 5 inatosha kwa ekari kwa msimu hadi mavuno)

SUMU YA KANITANGAZE

Sumu zinazopendekezwa  zaidi ni kama ifuatavyo!
Spidex 500 mls- 40,000  -50,000/=
Liberty 500 mls-??
Amsac 100 mls- 15,000- 20,000/=
Coragen??
Belt??
Multi-Alpha
Sumectin
Ruruka 100 gm- 5,000/=
Click??

SUMU ZA KUKINGA NA KUTIBU MAGONJWA YA FANGASI AU KUVU

Linkimil 72, Ivory 72, Wilthane, Snowsuccess, 1 kg: max. Price 20,000/=

BONYEZA HAPA: KUFAHAMU SUMU ZA MAGONJWA YA FANGASI AU KUVU 
Matumizi: 45 gm/20L za maji

Pulizia kila mara baada ya siku kati ya 7 hadi 14:

Gram 500 inatosha kwa ekari moja kwa mpigo mmoja

Nyanya huiva kwa muda wa siku 60 hadi 70: sawa na wiki 8 hadi 10.

Na huendelea kuwiva kwa muda wa miezi hadi 3. Mfano wa nyanya nzuri ni Ranger F1, Commando F1 au SIFA F1

Hivyo matumizi ya sumu za kuvu huendelea hata palemavuno yanapokuwa yanaendelea.

Miezi 3 (Siku 90 ) sawa na wiki 12

NADHANI KAMA MKULIMA UTAKUWA UMEPATA WALAU MWANGA JUU YA TATHIMINI YA GHARAMA ZA KILIMO CHA NYANYA.

GHARAMA AMBAZO HAZIJAJUMUISHWA:

1. Shamba
2. Kulima
3. Wafanyakazi
4. Umwagiliaji
5. Vifaa vya Shamba (Boot, Bomba/pump, majembe, rake, vifaa kinga, n.k)

NUNUA FORMULA ZA MBOLEA NA VIUATILIFU KWENYE KILIMO CHA NYANYA 


SOMA: MUONGOZO MFUPI  KILIMO BORA CHA NYANYA 

WASALAAM.
KWA MAWASILIANO

 Mr Mpinga +255 757 139 423.
Facebook: kilimo for life 
Instagram: kilimo for life 
Email: kilimoforlife@gmail.com 

PIGA SIMU KUULIZA JAMBO LOLOTE LINALOHUSU KILIMO NA SIYO VINGINEVYO.

MBEGU ZOTE ZINAPATIKANA

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho Maarufu