SABABU YA MAJANI YA NYANYA KUJIKUNJA SHAMBANI


KILIMO FOR LIFE ni moja ya mtandao wa kilimo unaoongoza kwa kusomwa na kupitiwa na wasomaji na waperuzi wengi zaidi.

Ni mtandao ulioanzishwa na
Mr A. Mpinga mwenye nia,dhamira na malengo ya kumsaidia Mkulima kunufaika na fursa ya kilimo kwa kumuwezesha kufahamu mbinu na namna bora zaidi ya kukiendea kilimo cha kitaalamu kwa kufuata Kanuni bora zaidi za Agronomia na Matumizi sahihi ya mbolea na viuatilifu pia kutoa tathmini ya gharama za kilimo cha mazao mbalimbali.


BONYEZA HAPA KUPATA FORMULA ZA KILIMO CHA MAZAO

Hapa tutaainisha sababu za tatizo mtambuka ambalo linawasumbuwa wakulima wengi nchini na duniani kwa ujumla kuhusiana na majani ya nyanya kujikunja pasina ya sababu inyoonekana.

Wakulima wengi wamekuwa wakisumbuka saana huhusiana na Tatizo hili. Na mara nyingi tumekuwa tukipigiwa simu kuulizwa tu kuhusiana na tatizo hili.

Hivyo ili kusaidia wakulima wote nchini; makala hii ambayo ni elimishi na yakitaalamu itafafanuwa kiufupi kuhusiana na tatizo hili na kubainisha namna ya kukabiliana nalo.

KARIBUNI
Imeandaliwa na Mr Mpinga +255 757 139 423.

Habari Mpendwa msomaji wa makàla zetu za kilimo cha mazao mbalimbali kupitia mtandao wetu wa Kilimo for life!

Mara nyingi kujikunja kwa majani ya mmea wa nyanya (kujikunja kuelekea juu au chini) husababishwa na Hali ya mazingira, kemikali, wadudu na magonjwa.

KUJIKUNJA KUNAKOSABABISHWA NA HALI YA KIMAZINGIRA.
Hii ni hutokea mara nyingi saana kwenye zao la nyanya na pilipili Hoho; husababishwa na Joto kali na umwagiliaji usio yakinifu.
Mkulima hapaswi kutishika/kupata hofu kutokana na hali hii kwasababu haidhuru wala kuathiri mavuno.
Hali hii Huendelea kwa siku kadhaa na hukoma mara tu Hali ya hewa inapokaa sawa.
Mmea hukunja majani yake (Leaf roll) ili kupunguza uso wa majani (leaf surface) kukabiliana na hali ya upungufu wa maji.

USHAURI: Mkulima ahakikishe anamwagilia maji ya kutosha na kulainisha udongo ili maji yafike kwenye mizizi yote.

Kujikunja kunakosababishwa na mazingira ya joto au upungufu wa maji 

Kujikunja kunakosababishwa na mazingira ya Joto au upungufu wa maji

KUJIKUNJA KUNAKOSABABISHWA NA WADUDU NA MAGONJWA.

Uwepo wa wadudu waharibifu wanaofyonza kwenye majani kama vile kimamba, Vithiripi na vipepeo weupe, husababisha kueneza magonjwa ya virusi.
Magonjwa ya virusi hayana tiba Mara yanapoingia na yanaathiri mavuno kwa kiwango kikubwa.

Majani yalioathiriwa na virusi kujikunja kwake ni tofauti na kujikunja kwa majani kulikosababishwa na mazingira. 
Kujikunja kwake huambatana na uvimbe uvimbe mdogo mdogo kwenye majani (leaf curling)
Pia kwenye Ugonjwa wa batobato (Tomato mosaic Virus) mishipa ya jani la Nyanya (leaf veins) kwa chini huwa na rangi ya zambarau (purple) kwa mbali.

Ugonjwa mwengine wa virusi (Tomato yellow leaf curl virus- TYLV) ambao huwa na dalili ya uwepo wa rangi ya umanjano kwenye majani.

Tomato yellow leaf curl virus 
MBEGU ZA TIKITI, NYANYA, PILIPILI HOHO, VITUNGUU N.K
Tomato mosaic virus
KUKABILIANA NA TATIZO HILI:
Dhibiti wadudu wasumbufu na waharibifu kwa kutumia viuatilifu sahihi mara tu ugunduapo uwepo wao.
Tumia Dudumectin, Duduacelamectin, Snowthunder, au liberate kuwadhibiti wadudu waharibifu.


NUNUA  FORMULA ZA MPANGILIO WA MBOLEA NA VIUATILIFU KWNEYE KILIMO CHA NYANYA 

KUJIKUNJA KUNAKOSABABISHWA NA KEMIKALI ZA KUUWA MAGUGU (HERBICIDES).
Utafiti unaonesha kuwa Shamba lililopuliziwa kemikali za viuwa gugu au kutumia mbolea za wanyama waliokula majani yaliyopuliziwa kemikali za viuwa gugu ni moja ya sababu ambazo ndivyo visababishi vya majani ya nyanya kujikunja.

Sababu hii ni vigumu kugundulika, hivyo si rahisi kujuwa namna ya kudhibiti tatizo hili.

MWISHO 

WASALAAM.

BONYEZA HAPA: KUFAHAMU SABABU YA ZAO LA NYANYA KUDODOSHA MAUWA

BONYEZA HAPA: KUSOMA MAKALA YA KILIMO BORA CHA ZAO LA NYANYA 

BONYEZA HAPA: KUFAHAMU UGONJWA HATARI WA KATA KIUNO


WASILIANA NASI KWA MSAADA NA USHAURI KUHUSIANA NA KILIMO CHA MAZAO YOTE.

MBEGU BORA AINA ZOTE ZINAPATIKANA.

PIGA SIMU:
+255 757 139 423 Mr A Mpinga.

Baruwa 
abbas.mpinga@continentalseeds.com

Instargram: kilimo for life 
Facebook: kilimo for life

BONYEZA HAPA UNGANA NA KILIMO FOR LIFE FARMERS WHATSAPP GROUP.

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho Maarufu