HASARA YA MATUNDA MENGI KWENYE KILA SHINA LA TIKITI MAJI.

JE NI FAIDA AU HASARA YA MATIKITI MENGI KWENYE SHINA MOJA??
AnitaF1 



KILIMO FOR LIFE ni mtandao pekee wa kilimo unaoongoza kwa kusomwa na kupitiwa na wasomaji na waperuzi wengi zaidi.


BONYEZA HAPA KUWASILIANA WHATSAPP

Ni mtandao ulioanzishwa na Mr A. Mpinga mwenye nia,dhamira
na malengo ya kumsaidia Mkulima kunufaika na fursa ya kilimo kwa kumuwezesha kufahamu mbinu na namna bora zaidi ya kukiendea kilimo cha kitaalamu kwa kufuata Kanuni bora zaidi za Agronomia na Matumizi sahihi ya mbolea na viuatilifu pia kutoa tathmini ya gharama za kilimo cha mazao mbalimbali.

Kilimo for life ikiendesha mafunzo ya kilimo bora kwenye vikundi vya wakulima mkoani Njombe

Tunamshauri na kumsaidia mkulima kupata mbegu bora na halisi (isiyo ghushi/Feki) pia kumsaidia mkulima kutatua changamoto zote zimkumbazo shambani.

HASARA YA KUACHA MATUNDA YA MATIKITI MENGI KWENYE SHINA MOJA.

Habari Mpendwa msomaji wa makàla zetu za kilimo cha mazao mbalimbali kupitia mtandao wetu wa Kilimo for life!

Leo tunapenda kujulisha Faida au Hasara ya Mkulima kufurahia uwingi wa matunda ya tikiti kwenye kila shina.

Wakulima wengi wanahamu na kufurahia uwingi wa matunda ya tikiti kwenye kila shina, Na ndiyo maana wengi kabla ya kununuwa mbegu huuliza, Je shina moja lina uwezo wa kuzaa matunda mangapi??

Hii ni dalili kuu ya wakulima wengi kuwa Na  hamu ya mavuno mengi ili kutengenezea Faida zaidi.

JE UKWELI NI UPI??
ukweli ni kuwa Hakuna Faida ya kuwa na matunda mengi kwenye kila shina la tikiti maji bali ni hasara pale unapoacha matunda mengi kwenye kila shina.

Hii ni kwasababu;
Endapo shina la tikiti maji linakuwa na matunda mengi (matatu na zaidi ) hii hufanya shina kukosa uwezo wa kulisha virutubisho linganifu / au vya kutosha katika kila tunda.

Athari yake hufanya mashina kuwa na matunda madogo madogo zaidi kuliko mashina yenye matunda ya tikiti machache (Moja hadi mawili)
Matunda mawili mawili kwenye kila shina lenye siku 58

BONYEZA HAPA KUFAHAMU MBEGU BORA ZAIDI ZA TIKITI MAJI TANZANIA 

Kumbuka kuwa: matunda madogo madogo hayavutii sokoni kwa kipindi hiki cha sasa Bali masoko ya sasa yanahitaji na yanapenda matikiti makubwa zaidi na yenye kuvutia.


Matunda mawili mawili yaliyoshamiri vyema kwenye kila shina.

Endapo shina likashindwa kulisha matunda yake ipasavyo; matunda yanakuwa madogo madogo na yenye maumbo mabaya yasiyovutia sokoni.

BONYEZA HAPA: SOMA MUONGOZO MFUPI WA KILIMO BORA CHA ZAO LA TIKITI MAJI 

Shina linapopunguziwa matunda na kubakiza matunda machache (moja hadi mawili) huwa na uwezo wa kulisha virutubisho vya kutosha katika kila tunda, hivyo kufanya matunda kuwa na Afya nzuri, Uzito mkubwa (kilo 8 hadi 12) na maumbo mazuri zaidi yenye kuvutia sokoni.

Matunda ya tikiti yanayovutia sokoni


MFANO
Familia yenye watoto wengi na chakula kichache huwa na watoto wasiyo na Afya nzuri.
Shina la tikiti linaposhindwa kugawa virutubisho vya kutosha katika kila tunda 

USHAURI
Tunashauri pindi mashina ya tikiti yanapoanza kutoa matunda, Mkulima apunguze matunda ya tikiti (yasiyovutia) kwenye kila shina na aache matunda (yenye Afya) yasiyozidi mawili (tunda moja katika kamba).



Pia mkulima anaweza kupunguza matawi yasiyo na tija ili virutubisho vielekezwe kwenye uzalishaji wa matunda ya tikiti.

Ekari moja ya zao la tikiti maji linatakiwa kuwa na mashina kuanzia 2666 hadi takribani 4500 kulingana na mfumo uliotumika kulima na nafasi zilizotumika.
Mkulima aliyevuna matikiti makubwa zaidi na yenye kuvutia: alisimamiwa na kilimo for life.
MBEGU BORA ZA TIKITI, NYANYA, VITUNGUU NA HOHO N.K
Ekari moja ya zao la tikiti maji inatakiwa itoe tani zaidi ya 40 za tikiti maji pale Mkulima akilima kitaalamu kwa kufuata Kanuni bora zaidi za Agronomia.

KUMBUKA: Kilimo for life tunatoa ushauri bure.

WASILIANA NASI 
+255 757 139 423 Mr A Mpinga Arusha 

E-mail 
kilimoforlife@gmail.com 

Facebook: kilimo for life 
Instargram: kilimo for life

BONYEZA HAPA UNGANA NA KILIMO FOR LIFE FARMERS WHATSAPP GROUP
NUNUA FORMULA YA MPANGILIO WA MBOLEA NA VIUATILIFU KWENYE KILIMO CHA TIKITI MAJI KWA MUONGOZO ZAIDI

Maoni

Machapisho Maarufu