UKWELI KUHUSU FAIDA KATIKA KILIMO CHA ZAO LA TIKITI MAJI.


JE FAIDA YA ZAO LA TIKITI MAJI IPO VIPI???

Na Mr Mpinga +255 757 139 423.


Leo napenda kujulisha uhalisia wa Faida ya zao la tikiti maji.

BONYEZA HAPA KUNUNUA FORMULA ZA MBOLEA KWENYE MAZAO

Wengi wamekuwa wakipaparukia kulima zao la tikiti kwa hamasa na mihemuko kutokana na kusikiliza wanayoyasema na kuyazuwa watu kuhusu zao la tikiti, Hivyo wengi wa wanaolima Tikiti kwa mara ya kwanza hulima kwa pupa na siyo kitaalamu na ndiyo maana wengi hutumbukia katika hasara kubwa.

NI VIPI UTAPATA FAIDA KATIKA KILIMO CHA ZAO LA TIKITI MAJI.

1. Chaguwa mbegu bora yenye ushindani sokoni
Huu ni Mfano wa mbegu nzuri ya Tikitimaji yenye uhitajio sokoni 

2. Chaguwa mbegu sahihi yenye mavuno mengi
Huu ni Mfano mzuri wa uzaaji wa zao la tikiti maji shambani.

3. Fuata kanuni sahihi za Agronomia kwa huduma na matunzo ya mazao shambani kwa kuzingatia matumizi sahihi ya mbolea na viuatilifu kwa wakati sahihi.

4. Chaguwa shamba sahihi na andaa miundombinu wezeshi katika zao la tikiti maji.

UFAFANUZI
Mbegu nzuri za tikiti maji, huzaa Tunda la uzito wa wastani Kilo 8 hadi 12

Shina la tikiti maji litazaa vizuri zaidi endapo litahudumiwa vizuri kwa kupata virutubisho linganifu tena kwa wakati sahihi

Mmea wa tikiti maji utazaa vizuri zaidi endapo Afya ya mmea itazingatiwa wakati wote ikiwemo kudhibiti magonjwa na wadudu waharibifu shambani.

Mbegu nzuri za tikiti hufanya tunda kuuzika kwa urahisi sokoni, kwani Tunda  huvutia kwa ukubwa, rangi ya Nje na ndani.

KUKOKOTOA FAIDA.

Kwa ekari moja yenye ukubwa wa mita square 4900

Kwa miundombinu niliyofundisha katika makala ya FAHAMU MBEGU BORA ZAIDI ZA TIKITI MAJI TANZANIA Utapata mashina kuanzia 4000 katika ekari moja.

Endapo katika kila shina la tikiti maji ukabakisha matunda Mawili au Moja, Kwa shina lililohudumiwa vizuri zaidi, utapata tunda lenye uzito wa Kilo 8 hadi 12

Endapo utabakisha tunda moja katika kila shina lililohudumiwa vizuri; uhakika wa ukubwa wa Tunda ni uzito wa Kilo kuanzia 10 na kuendelea.

Hivyo endapo utaacha Tunda moja moja tu katika kila shina lililohudumiwa vizuri utapata tunda lenye uzito wa Kilo kuanzia 8

Katika mashina 4000 utapata matunda 4000

Katika matunda 4000 yenye kilo 8 kwa kila tunda Jumla utakuwa na tani 36 kwa ekari Moja.

Kilo moja ya tikiti maji sokoni huuzwa kuanzia shilingi za kitanzania 300 na kuendelea

Hivyo kwa tani 36 utakuwa na 10, 800,000/=

Kwa wanaotumia miundombinu ya kawaida na kwa nafasi ya mita 2 kwa 1 kwa ekari Moja utapata miche  2450, na matunda 2450 sawa na tani 19.5
Ambapo ataingiza kiasi cha 5, 850,000/=


KUMBUKA: FAIDA NA HASARA NI SEHEMU YA KILIMO BIASHARA, HIZI NI HESABU ZA NADHARIA LAKINI ZIMETHIBITISHWA KWA VITENDO KWA WAKULIMA WALIOJIZATITI KULIMA KITAALAMU KWA KUFUATA KANUNI SAHIHI ZA AGRONOMIA KATIKA KILA HATUWA YA UKUAJI WA ZAO SHAMBANI.

ASANTENI

BONYEZA HAPA KWA MAHITAJI YA MBEGU AINA ZOTE

BONYEZA HAPA KUUNGANA NA KILIMOFORLIFE FARMERS GROUP  KWA MAHITAJI YA USHAURI KUHUSIANA NA KILIMO CHA MAZAO YOTE TANZANIA

WASILIANA NAMI KWA MSAADA ZAIDI

+255 757 139 423
kilimoforlife@gmail.com

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho Maarufu