MKULIMA ATATUMIAJE FURSA HII YA MVUWA NYINGI??

TUMIA FURSA HII YA MVUWA KUTENGENEZA FAIDA KATIKA KILIMO 

Na Mr Mpinga

Habari Mpendwa msomaji wa makàla zetu za kilimo cha mazao mbalimbali kupitia mtandao wetu wa Kilimo for life.

PATA FOMULA ZA MBOLEA NA VIUATILIFU KWENYE KILIMO CHA MAZAO YOTE 

BONYEZA HAPA KUNUNUA FORMULA ZA MBOLEA KWENYE MAZAO

Kilimo for life inakusudia kuhamasisha, kutaalamisha kwa  kufundisha wakulima kuwekeza kwenye kilimo biashara kwa kulima kitaalamu zaidi ikiwemo kuchaguwa mbegu bora kulingana na ukanda pia matumizi sahihi ya mbolea na viuatilifu kwa wakati sahihi.

Hapa nina kusudia kuwatonya jambo wakulima wangu;

Mvuwa inavyonyesha kwa wingi wakati huu; wakulima wengi huogopa kuanza kulima mazao ya mbogamboga; kuogopea kwamba Mvuwa nyingi huharibu mimea na ni kisababishi kikubwa cha visumbufu ikiwemo magonjwa, magugu na wadudu mashambani.

Hii yaweza kuwa ni Hoja ya msingi saana kuizingatia katika kilimo, lazima mkulima usiingie kichwamchunga katika miradi ya kilimo biashara na ndicho kisababishi cha wengi kuumbuka kwa kupata hasara kubwa.

UTATUMIAJE MVUWA HIZI KUTENGENEZA FAIDA KATIKA KILIMO CHAKO??

Kwa mazao yote ya mbogamboga yanayohitajia kitalu kisha kupandikizwa shambani; mfano Nyanya, pilipili Hoho, pilipili mbuzi, kichaa, n.k na wakulima wote wa green house.

Tumieni muda huu wa Mvuwa nyingi kuotesha miche yenu katika kitalu, ili mpaka miche inapokomaa na kuwa tayari kwa kupandikizwa shambani, kulingana na ukanda wetu wa Afrika ya mashariki tunataraji kupunguwa kukubwa kwa mvuwa ambapo ni Hali ya hewa afadhali/rafiki kwa kupandikiza miche shambani..!!

Kwa miche iliyokomaa vizuri, kitaalamu tunaamini kuwa inauwezo wa kukabiliana na mazingira yeyote hatarishi kama vile magonjwa, wadudu, magugu, upepo, Mvuwa, n.k

Hivyo kwakuwa Mvuwa zitakuwa zimepunguwa; mkulima atazingatia zaidi kukinga mmea dhidi ya mavamizi yeyote ya magonjwa na wadudu.

UTALINDAJE MICHE YAKO KITALUNI DHIDI YA MVUWA KALI 
Miche iliyochini ya uangalizi mkubwa 

Ninashauri mkulima kufunika kitalu chake kwa majani mengi au kufunika kwa nailoni yenye kupitisha mwanga kutoruhusu makali ya matone ya mvuwa yanayoweza kuathiri uotaji wa mbegu au miche kitaluni: kisha chimba mifereji mikubwa pembeni mwa kitalu kuelekeza maji ya mvuwa mbali na kitalu.
Kitalu kilichofunikwa kuepusha athari ya mazingira hatarishi ya nje. 

Hii itasaidia miche kukuwa vizuri na kwa usalama zaidi mpaka siku ya kupandikizwa shambani.

FAIDA INAKUJAJE??
Faida inakuja pale unapoanza kuvuna zao lako; pindi utakapoanza kuvuna mfano nyanya zako kutakuwa na bei nzuri sokoni kwani ni wakulima wachache ambao watakuwa wameshaanza kuvuna zao hilo, kwa maana halisi ni kwamba bado kutakuwa na uhaba wa bidhaa sokoni, na uhaba wa bidhaa sokoni ndiyo kielelezo cha bei nzuri ya bidhaa husika.

Kwa maana hiyo sasa; wakulima waliyelima mwanzoni katika mazingira magumu watauza mazao yao kwa bei nzuri tena bei faidishi kabisa.
Mavuno ya pilipili Hoho yakiambatana na soko zuri humtajirisha Mkulima 


Hivyo Mkulima atafaidi mradi wake zaidi kuliko yule aliyelima kipindi cha mazingira wezeshi ambapo kila mtu huanza kulima na kipindi cha kuvuna kila mtu huwa tayari kwa kuvuna hivyo bidhaa huwa nyingi zaidi sokoni na bei yake hushuka.

WASILIANA NAMI KWA MSAADA NA USHAURI KUHUSIANA NA KILIMO CHA MAZAO.

+255 757 139 423 MR MPINGA AGRONOMIST 
Kilimoforlife@gmail.com 
istargram: kilimo for life 
Facebook: Abbas Mpinga 

BONYEZA HAPA KUJIUNGA NA GROUP LA WHATSAPP 

BONYEZA HAPA KWA MAHITAJI YA MBEGU AINA ZOTE KWA GHARAMA RAFIKI KWA WAKULIMA

Maoni

Machapisho Maarufu