mbegu bora ya nyanya kwenye green house

MBEGU YA NYANYA KWENYE GREEN HOUSE 

Na Mr Mpinga 
+255 757 139 423
Kilimoforlife@gmail.com

Habari Mpendwa msomaji wa makàla zetu za kilimo cha mazao mbalimbali kupitia mtandao wetu wa Kilimo for life

Kilimo for life inakusudia kuhamasisha na kufundisha wakulima kuwekeza kwenye kilimo biashara kwa kulima kitaalamu zaidi kwa kuzingatia uchaguzi sahihi wa mbegu bora kulingana na ukanda pia matumizi sahihi ya mbolea na viuatilifu kwa wakati sahihi na zaidi ni kufuata kanuni bora za Agronomia kwa matunzo ya mazao shambani.

Kama tulivyokwisha ainisha juu ya mambo ya kuzingatia katika kilimo bora chenye faida cha zao la Nyanya, leo Tutaielezea mbegu bora zaidi za Nyanya inayopatikana Tanzania ya Anna F1. 

NUNUA FORMULA YA KILIMO BORA CHA NYANYA KUPATA MPANGILIO HALISI WA MBOLEA NA VIUATILIFU 

Nimeamuwa kuielezea Anna F1 kwasababu, Nilipata kualikwa kutembelea na kukaguwa Mashamba katika  green house 50 za kampuni ya PASS zilizopo Morogoro Mjini. Nilikutana na Changamoto za kuhusu ukweli, uhakika mbegu ile na uhalisia wake. Baada ya kukaguwa niligunduwa kuwa ni green house mbili tu zilikuwa na mbegu sahihi na halisi. Hiini ilisababishwa kampuni kununuwa miche badala ya Mbegu.

Mashina yale yalikuwa yanazaa Nyanya ndogondogo na cluster zenye nyanya 3 hadi 4 pekee: hiki ndicho kilicho nisumbuwa na kunishawishi kuandika makala maalumu kuihusu Anna F1. Lengo ni kusaidia na kuelimisha wakulima wakubwa na wadogo juu ya kilimo cha kitaalamu chenye tija na kuepusha udanganyifu.

KARIBUNI

STEVE F1

  • Ni Mbegu inayorefuka kwenda juu hivyo kupelekea ulazima wa kuwekewa miti au kamba (stacking).
  • Mbegu ya steve ni mbegu inayozaa zaidi kuliko aina yeyote pale inapohudumiwa vizuri 
  • Mbegu ya Steve F1 hutoa Nyanya zenye uzito wa 180 hadi 200 gm 
  • Imavumilia baridi kali na joto pia
  • Inastahimili saana magonjwa ya ukungu 
ANNA F1
Hii ni mbegu inayofanya vizuri zaidi kanda zote na ni mbegu ambayo umekuwa chaguo la awali zaidi kwa wakulima wanaolima katika kitalu nyumba (Green House).
Anna F1 ikiwa kwenye shamba la nje 

Ni Mbegu inayorefuka zaidi kwenda juu hivyo kupelekea ulazima wa kuwekewa miti au kamba (stacking).

Mbegu ya Anna F1 ni mbegu inayozaa saana

Anna F1 ikiwa katikà hatuwa ya uzaaji

MBEGU BORA ZA TIKITI, VITUNGUU, NYANYA, HOHO, N.K 

Mbegu ya Anna F1 hutoa Nyanya zenye uzito wa 150 hadi 170 gm 

Anna F1 hutoa Mkungu (Cluster) wenye Nyanya 9 hadi 18 Hii ni kutokana na kwamba inauwezo wa kutoa mikungu pacha pacha 

Anna F1 ikiwa na matunda 9 kwenye Mkungu mmoja uzito pacha

Anna F1 ina shina nene lenye kushika vizuri kwenye udongo 

KUMBUKA: Anna F1 Inafaa pia kupanda katika mazingira ya Nje yaani Open field kwa atakaeweza kumudu kugharamikia miti yaani stacking pia mtandao yaani mulching ni muhimu zaidi kwa wanaolima nje.

BONYEZA HAPA KUULIZA UPATIKANAJI WA MBEGU NA MBOLEA AINA ZOTE 

KWA MAELEZO ZAIDI

KUUNGANA NA KILIMO FOR LIFE FARMERS GROUP KUULIZA MASWALI KUHUSIANA NA KILIMO CHA MAZAO.

AU

WASILIANA NASI 
+255 757 139 423 
Kilimoforlife@gmail.com 

Maoni

Machapisho Maarufu