FAHAMU MBEGU BORA ZAIDI ZA VITUNGUU TANZANIA
FAHAMU MBEGU BORA ZAIDI ZA VITUNGUU TANZANIA
Na Mr Mpinga
+255 757 139 423
Habari Mpendwa msomaji wa makàla zetu za kilimo cha mazao mbalimbali kupitia mtandao wetu wa Kilimo for life
Kilimo for life inakusudia kuhamasisha na kufundisha wakulima kuwekeza kwenye kilimo biashara kwa kulima kitaalamu zaidi kwa kuzingatia uchaguzi sahihi wa mbegu bora kulingana na ukanda pia matumizi sahihi ya mbolea na viuatilifu kwa wakati sahihi na zaidi ni kufuata kanuni bora za Agronomia kwa matunzo ya mazao shambani.
Kama tulivyokwisha ainisha juu ya mambo ya kuzingatia katika kilimo bora chenye faida cha zao la Kitunguu maji, leo tutaorodhesha mbegu bora zaidi za Vitunguumaji zinazopatikana Tanzania.
1. JAMBAR F1
Hii ni mbegu inayofanya vizuri zaidi mazingira ya joto na Joto la wastani.
Ina rangi nyekundu iliyokolea
Ipo tayari kuvunwa baada ya siku 85 hadi 95 baada ya kupandikizwa
Hutoa tani 23 kwa ekari moja
SV 7030 F1
Hii ni mbegu inayofanya vizuri zaidi mazingira ya Baridi na Joto la wastani
Ina rangi nyekundu inayong'aa
Ipo tayari kuvunwa siku 75 baada ya kupandikizwa
Hutoa tani 23 kwa ekari moja
Hudumu muda mrefu (miezi 6) bila kuharibika
Shape yake ni nzuri zaidi na wala haitoi vipacha
NEPTUNE F1
Hii ni mbegu inayofanya vizuri mazingira ya Baridi na Joto
Inakuwa haraka haraka na ina majani mengi yenye kuvutia
Ina rangi nyekundu Mpauko
Ipo tayari kuvunwa siku 95 hadi 100 baada ya kupandikizwa
Hutoa tani hadi 40 kwa ekari moja
Hudumu muda mrefu bila kuharibika
Shape yake ni nzuri haitoi vipacha
Size yake ni kubwa zaidi kuliko kitunguu chochote
Mavuno ya Mbegu ya Neptune F1 katika shamba darasa Arusha |
MBEGU ZINGINE NI
Red Bombay, Red creole, Super Red Bombay, Mang'ola, Mang'ola red n.k
Hizi ni mbegu zenye mavuno ya wastani na mbegu zake ni rahisi kuzalishwa na huzalishwa maeneo mbalimbali hata Nchini.
Ni Mbegu zinazolimwa zaidi Afrika kwasababu ni mbegu rahisi zenye gharama za chini.
Tunawashauri wakulima kuwekeza kwenye kilimo biashara kwa kulima kitaalamu zaidi ikiwemo kuchaguwa mbegu bora kulingana na ukanda zenye mavuno mengi na zenye kukubalika sokoni.
KUJIUNGA NA GROUP LA KILIMO FOR LIFE FARMERS GROUP KWA MUONGOZO ZAIDI SHAMBANI BONYEZA HAPA
WASILIANA NASI KWA MSAADA NA USHAURI KUHUSIANA NA KILIMO CHA MAZAO YOTE TANZANIA
+255 757 139 423 MR MPINGA
kilimoforlife@gmail.com
Maoni
Chapisha Maoni