Fahamu ugonjwa wa Ubwiru chini kwenye Tikiti maji (Downy mildew in water melon)
UGONJWA WA UBWIRU CHINI KWENYE TIKITI MAJI
(DOWNY MILDEW IN WATER MELON)
Na Mr Mpinga
+255 757 139 423.
Ubwiru chini (Downy mildew) Ni miongoni mwa magonjwa ya
Kuvu hatari kwenye mazao jamii ya cucurbit Mfano Tikiti Ambao hutokea zaidi kipindi cha msimu wa Joto
Kuvu hatari kwenye mazao jamii ya cucurbit Mfano Tikiti Ambao hutokea zaidi kipindi cha msimu wa Joto
Athari zake hutokea zaidi kwenye majani na huwa hauathiri Matunda ya tikiti.
Mazingira wezeshi ya ugonjwa huu ni;
1⃣Hali ya Ubaridi (16 °C Usiku na 21°C Mchana)
2⃣Hali ya Umajimaji wa kudumu shambani
3⃣Mbanano wa mimea shambani n.k
DALILI
1⃣Kuwepo kwa Madoa rangi ya brown juu ya majani
2⃣Kuwepo kwa madoa ya rangi ya zambarau kolevu (Dark puple) chini ya majani.
2⃣Kuwepo kwa milainiko yenye muonekano wa majimaji kwa ndani (water lesions) chini ya majani
3⃣Majani ya tikiti kuanza kukauka na kupukutika kidogokidogo.
ATHARI
⏏kutokana na Majani kukauka na kupukutika kutokana na ubwiru chini: shina la tikiti hushindwa kuzalisha matunda mazuri yenye Afya.
⏏Mmea kukauka na kushindwa kuendelea kukuwa, kuzalisha na kustahimili mazingira
KUDHIBITI/KUKINGA.
1⃣Kuepuka kumwagilia maji kwenye majani ya mmea wa tikiti; Mkulima achaguwe miundombinu wezeshi katika umwagiliaji.
2⃣Kuepuka kupanda matikiti chini ya kivuli kuepuka mazingira ya Ubaridi
3⃣Mkulima anashauriwa kutumia viuatilifu vyenye mchanganyiko wa Chlorothalonil au Mancozeb ambavyo vinauwezo wa kukinga Ugonjwa huu hatari.
4⃣Endapo ugonjwa umeshagundulika shambani; Mkulima Atumie kiuwakuvu mfano kiwatilifu chenye mchanganyiko wa metalaxy au Dimethomorph, Carbendazim, Difeconazole, n.k
KUMBUKA: Puliza dawa ya kukinga Ugonjwa huu hatari kila baada ya siku 5 hadi 7.
Pia Hakuna aina ya Tofauti ya Mbegu ya tikiti yenye uwezo wa kukinzana na Ugonjwa huu wa Ubwiru chini.
MWISHO
KWA MAELEZO YA ZIADA
WASILIANA NASI
☎+255 757 139 423/717 439 423
✉kilimoforlife@gmail.com
BLOG
www.kilimoforlifetz.blogspot.com
Maoni
Chapisha Maoni