Fahamu ugonjwa wa kata kiuno (Damping off) na udhibiti wake
UGONJWA WA KATA KIUNO (DAMPING OFF) KWENYE MAZAO YA BUSTANI
Na Mr Mpinga
+255 757 139 423
kilimoforlife@gmail.com
Ugonjwa wa Kata kiuno/kinyausi au kwa kingereza Damping off ni
ugonjwa hatari Unaosababishwa na uwepo wa vimelea kuvu (Fangasi) wa Ardhini kwenye Udongo Mfano Spishi za rhizoctonia, fusarium, phytophthora na Pithium.
ugonjwa hatari Unaosababishwa na uwepo wa vimelea kuvu (Fangasi) wa Ardhini kwenye Udongo Mfano Spishi za rhizoctonia, fusarium, phytophthora na Pithium.
Ni ugonjwa unaoathiri mbegu au miche ya mazao hasa jamii ya mbogamboga kabla na mara baada ya kuota mfano Nyanya, vitunguu, Tikiti, mchicha, n.k
MAZINGIRA AMBUKIZI.
▶Kata kiuno hutokea zaidi katika kitalu chenye umajimaji (high moisture and humidity) muda mrefu na hali ya ubaridi
▶Mbanano/msongamano wa miche kwenye kitalu (Crowding)
DALILI
▶Kuanguka kwa miche kitaluni
▶Mbegu kutokuota vyema
▶Mizizi kuoza
▶Shina kuoza kwa chini
▶Miche kuwa na hali ya kuunguwa kwa juu kwenda chini (vitunguu)
▶Kuwa na mabaka yenye hali ya umajimaji
TIBA/KINGA
Ugonjwaa huu hauna tiba mara utokeapo kitaluni
KINGA
▶Tibu udongo kwa kuusafisha (sterilize) kwa njia ya Mvuke (steaming,Solarization.k) au kwa viuatilifu kama vile Blue copper n.k (Drenching)
▶Epuka/ Punguza kumwagilia kila nyakati za Jioni
▶Pulizia kitalu sumu ya kukinga Ugonjwa wa kuvu mara miche iotapo. Mfano Carbendazkm,Dimethomorph, Mancozeb 80 WP au Metalaxy n.k
Mfano wa sumu hizo ni Ridomil, Innovex, Farmerzeb, Ridomil, snow success, Xantho, Misters, oshothane n.k .
MWISHO
WASILIANA NASI KWA MSAADA NA USHAURI
☎+255 757 139 423/717 439423
✉kilimoforlife@gmail.com
BLOG
www.kilimoforlife.com
Maoni
Chapisha Maoni