MBEGU BORA ZAIDI ZA TIKITI MAJI TANZANIA
Habari Mpendwa msomaji wa makàla zetu za kilimo cha mazao mbalimbali kupitia mtandao wetu wa Kilimo for life
Kilimo for life inakusudia kuhamasisha na kufundisha wakulima kuwekeza kwenye kilimo biashara kwa kulima kitaalamu zaidi kwa kuzingatia uchaguzi sahihi wa mbegu bora kulingana na ukanda pia matumizi sahihi ya mbolea na viuatilifu kwa wakati sahihi na zaidi ni kufuata kanuni bora za Agronomia kwa matunzo ya mazao shambani.
Kama tulivyokwisha ainisha juu ya mambo ya kuzingatia katika kilimo bora chenye faida cha zao la tikiti maji, leo tutaorodhesha mbegu bora zaidi za tikiti maji zinazopatikana Tanzania.
Lengo ni kusaidia wakulima wetu wafahamu mbegu bora kulingana na soko lililopo ili waweze kunufaika na kilimo chao.
1. ANITA F1
Hii ni mbegu inayofanya vizuri zaidi nyakati zote kwa kanda zote
Ina rangi ya zebra kwa juu
Inastahimili Hali zote za mazingira (JOTO na BARIDI)
Inazaa kwa haraka zaidi siku 75
Inazaa tunda la uzito wa Kilo 8 hadi 12
2 SHABIKI F1
Hii ni mbegu inayofanya vizuri zaidi nyakati zote kwa kanda zote
Inastahimili Hali zote za mazingira (JOTO na BARIDI)
Inazaa kwa siku 80
Inazaa tunda la uzito wa Kilo 8 hadi 15
3.SUKARI F1 F1 F1
Hii ni mbegu inayofanya vizuri kwa kanda zote (JOTO na BARIDI)
Ina Rangi ya zebra kwa juu
Tunda lake Lina shape ya duara Butu (duara iliyorefuka)
Inazaa kwa muda wa siku 75 hadi 80
Inazaa Tunda la uzito wa Kilo 8 hadi 12
4. ASALI F1
Hii ni mbegu inayofanya vizuri kwa kanda zote (JOTO na BARIDI)
Ina Rangi ya zebra Mpauko kwa juu
Umbo la Tunda ni duara
Tunda lake ni tamu sana
Inazaa kwa muda wa siku 80
Inazaa Tunda la uzito wa Kilo 8 hadi 15
PATO F1
Hii ni mbegu nzuri kwa kanda zote
Ina Rangi ya zebra kwa juu
Inazaa kwa muda wa siku 80 hadi 85
Inazaa Tunda la uzito wa Kilo 8 hadi 10
KUMBUKA: Mbegu zote ni Bora na zimethibitishwa na Ofisi ya Taasisi ya kuthibitisha ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI).
PIA, kuna Aina nyingi zaidi za mbegu za tikiti ambazo hatujaziorodhesha hapo juu; Hili tumezingatia mbegu bora na shindani kulingana na uhitaji Sokoni
Mbegu zingine ni
Zebra F1
Sugarking F1
Sugar queen F1
Mkombozi F1
Apoorva F1
ZAIDI
KWA USHAURI NA MAHITAJI YA MBEGU NA BIDHAA ZOTE ZA KILIMO
WASILIANA NA KILIMO FOR LIFE KWA MSAADA ZAIDI
Simu: +255 757 139 423
Au
Baruwa pepe: Kilimoforlife@gmail.com
INSTAGRAM- Kilimo for life
FACEBOOK: Kilimo for life au Abbas Mpinga
Enter your comment...
JibuFutaAsante sana kiongozi. tunaomba tuone uwezo wakutoa matunda kwa kila aina ya mbegu apo juu. kwa mkulima Mavuno ndo key performance indicator.
Nashukuru
Vizuri sana mtalaam kwa somo fupi na nzuri.
JibuFutaElimi nzuri sana hongereni kwa maono makubwa
JibuFutaLakini mbona tunajiunga kwenye kundi la whatsap halikubali? Lakini pia mko sehemu gani ya Tanzania? Vp kuhusu bei ya hizo mbegu? Pia ni mbegu gani ambayo ni mpya zaidi sokoni ukilinganisha na Hali ya hewa ya sasa?