FAHAMU GHARAMA KATIKA KILIMO CHA NYANYA
MPANGILIO HAFIFU WA GHARAMA KATIKA
KILIMO CHA NYANYA TANZANIA
Na Mr. MPINGA
Hapa nitaelezea,
kujulisha, kuainisha, na kudadavuwa juu ya gharama za kilimo cha nyanya kwa
uchache Zaidi.
kulingana na utofauti
wa kikanda na mazingira, nitajulisha gharama za manejimenti ya shamba pekee;
yaani gharama za mbegu, madawa na mbolea zinazohitajika kwenye shamba la nyanya
kuanzia mwanzo hadi mavuno.
Gharama za kodi ya
shamba, umwagiliaji, wafanyakazi na miundombinu ya shambani haitoainishwa
kulingana na kutofautiana kwa gharama hizi kulingana na eneo au ukanda husika.
Gharama hizi zitakuwa
kwa eneo la ekari moja pekee
Hii itasaidia mkulima
kufahamu, kujuwa na kupanga bajeti ya ujumla kabla ya kuanza mradi wa kilimo
cha nyanya.
Ikumbukwe kuwa; zao
la nyanya shambani ni Zaidi ya mtoto mchanga katika malezi na matunzo; zao la
nyanya linahitaji umakini mkubwa sana katika kipindi chote cha ukuwaji mpaka
hadi mavuno. Maana hii ni kwamba; Smkulima anapaswa kutembelea na kujuwa hali
na maendeleo ya ukuwaji wa shamba kila siku.
MABEGU BORA ZA NYANYA
NA GHARAMA ZAKE
JINA LA MBEGU
|
KIASI KWA EKARI
|
BEI YA MBEGU
|
AINA
|
MSIMU/HALI YA HEWA
|
COMMANDO F1
|
30-40 gm
|
240000
|
MSHUMAA
|
BARIDI/MVUWA NYINGI
|
SIFA F1
|
30 gm
|
330000
|
MSHUMAA
|
JOTO/ MVUWA CHACHE
|
RANGER F1
|
30 gm
|
330000
|
MSHUMAA
|
JOTO,MNYAUKO, BARIDI, MVUWA NYINGI
|
SIFA F1
|
30 gm
|
MSHUMAA
|
MAZINGIRA YOTE
|
MADAWA YA UKUNGU NA GHARAMA
ZAKE KWA EKARI MOJWA
madawa ya kudhibiti magonjwa ya fangasi/ukungu/barafu/kuvu hupaswa kupigwa mara zaidi shambani kuliko madawa ya wadudu.
mkulima anapaswa kupiga madawa ya fangasi kila baada ya siku 7 hadi 14, kulinagana na ahali aya hewa.
kwa kipindi cha mvuwa nyingi; mkulima atapaswa kupiga dawa kila baada ya siku 7.
ni vyema kupiga dawa ya kukinga au kutibu na kukinga kabla ugonjwa haujaonekana au kutokea.
kwa mantiki hiyo ni kwamba waweza tumia dawa yeyote kati ya hizi zilizoorodheshwa chini kwa kukinga.
na kama ugonjwa umekwisha ingia; itabidi upige dawa ya kukinga na kutibu.
GHARAMA ZA MADAWA YA WADUDU.
Wadudu wasumbufu Zaidi
kwenye zao la nyanya namba moja ni KANITANGAZE, ikifuatiwa na vipepeo weupe,
vimamba, leaf miners n.k
Wadudu hawa
hudhibitiwa vizuri Zaidi kwa kupiga dawa mchanganyiko wa dudumectin au wilcron
na wiltigo plus.
Wiltigo plus inauwezo
mkubwa Zaidi wa kumdhibiti kanitangaze kwani hutoa kinga ya muda mrefu Zaidi (siku
21).
Hivyo ninawashauri wakulima kutumia Amsac, Liberity, belt, Couragen kuanzia mara tu utakapopandikiza miche shambani mpaka hadi mavuno.
Changanya kiasi cha 5 mls wiltigo plus na 30 mls dudumectin au wilcron katika lita 16 hadi 20 za maji.
Kumbuka kupiga dawa ya wiltigo plus kila baada ya siku 14-21 ili kuweka kinga dhidi ya kanitangaze,mdudu hatari Zaidi kwa zao la nyanya.
GHARAMA ZA MBOLEA
KATIKA ZAO LA NYANYA.
MUDA BAADA YA KUPANDIKIZA
|
MBOLEA
|
KIASI KWA EKARI
|
GHARAMA
|
WIKI 1-2
|
DAP (bora)
|
50 Kg
|
66,000- 67,000
|
YARAMILA OTESHA (bora Zaidi)
|
50 Kg
|
63,000-65,000
|
|
YARAMILA WINNER
|
50 Kg
|
65,000 – 68,000
|
|
WIKI 3-4
|
YARAMILA WINNER (bora Zaidi)
|
50 Kg
|
65,000 – 68,000
|
YARAVERA AMIDAS
|
50 kg
|
57,000 -58,000
|
|
UREA
|
50 Kg
|
56,000
|
|
NPK (bora)
|
50 Kg
|
59,000-61,000/=
|
|
MAUWA YA KIKARIBIA KUTOKA
|
YARALIVA NITRABOR (bora Zaidi)
|
50 kg
|
70,000-74,000/=
|
CAN
|
50 kg
|
43,000-45,000/=
|
|
MATUNDA YAKITOKA
|
YARALIVA NITRABOR+ NPK/ WINNER
|
25 Kg : 50 kg
|
35,000 +
59,000/68,000/=
|
BAADA YA MCHUMO WA KWANZA
|
YARALIVA NITRABOR+ NPK/ WINNER
|
25 Kg : 50 kg
|
35,000 +
59,000/68,000/=
|
MAELEZO: katika
orodha tajwa ya mbolea hapo juu, mbolea zote ni bora Zaidi kutumika nimezipaka kwa
rangi ya njano.
NB: mbolea ya samadi
haijainishwa kutokana na utofauti wa gharama kulingana na eneo.
Ni bora Zaidi kutumia
mbolea ya samadi kabla ya kupandikiza miche shambani.
Hivyo kwa Makala hii
gharzima mkulima ataamuwa atumie mbegu ipi, dawa zipi, na mbolea zipi kwa ghaarama
ipi ili kufanikisha mradi mzima wa kilimo cha nyanya.
Shukrani sana kwa
kusoma Makala zangu.
KWA USHAURI NA
MAHITAJI YA MBEGU, MBOLEA N.K WASILIANA NAMI
WASILIANA NAMI KWA 0757 139 423 Mr
Mpinga Agronomist na mshauri wa masuala ya kilimo
kilimoforlife@gmail.com
Hongera mtaalam, umetoa mfafanuzi mzuri
JibuFutaMaoni haya yameondolewa na mwandishi.
JibuFutaNashukuru kwa masomo yenu. Je naweza kutumiwa watsap?
JibuFutaNamba yangu,0687987724
Ahsante sana..vipi nyanya au mbengu nzuri ya kulima kwenye mkoa wenye mvua nyingi kama Kagera
JibuFuta