Angalia namna utakavyoweza kuandaa kuotesha mbegu za pasheni (karakara)

NAMNA YA KUANDAA MBEGU ZA PASHENI/KARAKARA.


Habari yako mpenzi msomaji wa makala zangu za kilimo cha mazao mbalimbali kupitia mtandao wetu wa kilimo for life.



Naandaa makala fupi juu ya uandaaji wa mbegu za pasheni.


1. Tafuta Tunda la PASHENI lililowiva vizuri.

2. Kata tunda la pasheni katikati kwa kisu kisha toa mbegu zilizomo ndani.



3. Osha mbegu za karakara vizuri katika maji ya moto au juice ya machungwa kwa saa 24 mpaka hadi nyama na rangu ya pasheni iishe kabisa..


4. Ziweke mbegu juu ya kitambaa au taulo safi zikauke.



5. Anika mbegu hizo katika taulo zikauke vizuri kwa mwanga wa jua kwa siku 3 hadi 4 kabla ya kuziloweka tena katika maji na kuzikausha kivulini.


6. Anzisha kitalu ktk kontena/visado kwa kuchanganya mchanga, Udongo wa juu (wenye rutba) na mbolea ya samadi kwa ujazo wa sentimita 10.


7. Kama kitalu chako ni cha tuta, tengeneza vituta vidogo katika kitalu vyenye umbali wa sentimita 5 ili kuzuia mbegu kuharibiwa  na maji

8. Sia mbegu katika tuta kwa umbali/ nafasi ya sentimita moja hadi 3

9. Tia maji katika kitalu kwa uhakika wa unyevu unyevu muda wote.

10. Mbegu huota baada ya wastani wa siku 20

11. Baada ya kuota, pandikiza mmea shambani ukifikisha urefu wa sentimita 27 hadi 30.

Kwa maelezo yote ya kilimo cha Pasheni Bonyeza HAPA

ASANTENI.

WASILIANA NASI

+255 757 139 423 Mr Mpinga

JIUNGE NA GROUP LA KILIMO FOR LIFE FARMERS GROUP KWA MUONGOZO ZAIDI

https://chat.whatsapp.com/HhTw8NzlzAhLfZBH6QImqE

Maoni

Machapisho Maarufu