Mbegu bora za mahindi kulingana na ukanda husika nchini Tanzania
Makala hii ni maalumu kwa ajili ya kumjuza mkulima juu ya aina ya mbegu za mahindi zinayoweza kukuwa kulingana na ecologia ya hapa nchini Tanzania.
1. Mbegu zinazotumika Nyanda za Juu Kusini
Maeneo ya mwinuko wa juu/ukanda wa juu (mita 1500-2300 kutoka usawa wa bahari): UH 6303, UH
615, UHS5350, PAN691, H625, H628, H614D, composite TMV-2, MERU 623, SC719, MERU IR621
• Ukanda wa kati (mita1000-1500 kutoka usawa wa bahari):
UH615, UH6303, UHS 401, UHS 5350, SC 627, H12
PAN69, COMPOSITE TMV-2, Staha-ST, Kilima- ST, MERU HB 513, MERU 515, STUKA1, n.k
• Ukanda wa chini (chini ya mita 1000 kutoka usawa wa bahari):
TMV-1, Staha-ST, Kilima-ST, Kito, SC
403, Situka M, UHS 401, MERU 513, MERU 405, H 12 N.k
• Miinuko aina zote UHS 401
Kama wakulima wamejiandaa kutunza mbegu kutoka katika mbegu ya kundi la mchanganyiko
mzunguko wa 1 na hata 2, mimea ambayo siyo mizuri inatakiwa kung’olewa kabla mahindi
hayajachanua na mahindi mazuri yachaguliwe ili kupata mbegu bora kutoka katika mimea yenye afya
wakati wa kuvuna. Hata hivyo mkulima kabla hajajaribu kutunza mbegu anatakiwa kupata ushauri
kutoka kwa bwana shamba.
TOSCI ni chombo cha serikali kinachoratibu na kusimamia ubora wa mbegu za mahindi zinazo tumika
hapa Tanzania.
Tusaidieni kwa kweli
JibuFuta