Kilimo cha matunda ya pasheni,pesheni au Karakara (Passion fruit) Tanzania na faida zake

KILIMO CHA MATUNDA YA PASHENI(KARAKARA)




Habari ndugu msomaji wa makala zangu za kilimo cha mazao mbalimbali kupitia mtandao wetu wa kilimo for life. Leo napenda kuelezea  fursa ya kilimo cha kisasa cha zao la matunda ya pasheni au pesheni au karakara nchini Tanzania.

Kilimo cha matunda ya Pasheni ni mojawapo ya fursa muhimu, nzuri na rahisi kwa uhakika wa kukuingizia kipato wewe mkulima kwa kipindi kirefu,  hii ni kutokana na ukweli kuwa soko la pasheni  ndani na nje ya nchi linakuwa kwa kasi kutokana na uhitaji na faida za tunda lenyewe na pia Juisi yake katka mwili wa binadamu.

UTANGULIZI.
Karakara/Pasheni au Passion fruit, kitaalamu Passiflora edulis ni mmea jamii ya miti ya matunda wenye tabia ya:

  • kutambaa, kujiviringisha.
  • Unakua katika maeneo ya tropiki na nusu-tropiki
  • unazaa matunda ya ukubwa wa yai.
  • Matunda yana rani ya Njano au Zambarau yenye kunukia vizuri.
HALI YA HEWA
  • Karakara hustawi katika usawa wa bahari  mpaka mita 2000 .
  • Hustawi vizuri katika wastani wa nyuzi joto 23-27 sentidredi
  • kiwango cha wastani cha mvua ni 800 mm hadi 1700 mm
  • pH ya Udongo ni 5.5 -6.5 na udongo mzuri ni wa mchanganyiko kichanga na kifinyanzi (tifutifu)
AINA ZA PASHENI/KARAKARA.
Kuna aina kuu 2 za Karakara ambazo ni Njano na Zambarau.
Matunda huwa kijani yawapo machanga na hubadilika yanapozidi ku.

Aina ya Njano






Huwa na matunda makubwa zaidi na  mashina yake ni makubwa zaidi.
Aina ya Njano hupendelea na hukua vizuri katika maeneo ya mwinuko wa chini na joto (tropiki) .
huanza kuzaa miezi 12 baada ya kupandwa na huzaa kwa wingi sana. Matunda ya Pesheni hukomaa na kuiva siku 80 baada ya Ua kuchavushwa.

Aina ya Zambarau






Matunda huwa madogo zaidi yenye uchachu kidogo, utamu, juisi nyingi na hunukia Vizuri zaidi.
Aina ya Zambarau hupendelea mwinuko kiasi mpaka wa juu takribani mita 2000 na hali ya baridi kiasi.
Aina ya Zambarau hukua haraka na huzaa miezi 7 mpaka 9 mara baada ya kupandwa.
Aina hii huwa na vipindi viwili vya mavuno ya juu kwa mwaka hasa miezi ya Julai na Januari.

UPANDAJI NA MPANGILIO WA SHAMBA:
Pesheni hupandwa kwa kutumia mbegu. Chagua matunda bora yaliyokomaa na kuiva vizuri kisha toa mbegu zake.

JINSI YA KUANDAA MBEGU ZA PASHENI/KARAKARA

 Panda mbegu katika tuta lililoandaliwa vizuri au kwenye viriba/mifuko iliyojazwa udongo uliochanganywa na mchanga kidogo na mbolea ya samadi. Mbegu huota na kuchipua wiki 2 mpaka 3 baada ya kupandwa. Mbegu zilizohifadhiwa muda mrefu huchelewa kuota na uotaji wake huwa wa chini.


Miche hupandikizwa shambani ikifikia kimo cha sentimita 25 hadi 30.
Chimba Mashimo yenye ukubwa wa sentimita 30 hadi 45 urefu, upana  na kimo,.

NAFASI (SPACING)






Achanisha nafasi ya mita 3 baina ya mmea katika mstari na mita 1.8 hadi 2 baina ya mstari na mstari.

Panda miche katika mashimo yenye udongo uliochanganywa na samadi au mboji vizuri.
kuongeza mbolea ya chumvichumvi ya kupandia na kukuzia ni bora zaidi.

STAKING






Tumia nguzo urefu wa wastani mita 1.5 hadi 2 juu ya ardhi kufuata mistari zikipishana mita 6 mpaka 9 na unganisha kwa waya au kamba imara. Nguzo zaweza kuwa za chuma au mti kulingana na uwezo wa mkulima mwenyewe.
Miche inaporefuka ielekeze vizuri kwa kuishikiza au kuiviringisha kuelekea juu kuushika waya/kamba ya juu ili itambae juu yake vizuri.

KUVUNA.
Karakara huwa tayari kuvunwa pindi linapobadilika rangi kwenda kwenye umanjano halisia au rangi ya zambarau ambapo kikonyo hukauka na
Matunda yaliyokomaa na kuiva huanguka chini yenyewe.
Mavuno kwa mwaka katika shamba lililotunzwa vizuri huwa kati ya tani 9 mpaka 15 kwa hekta,  hivyo kwa nusu hekta (mita 50 urefu kwa 50 upana)  utapata kati ya tani 4.5 mpaka 7.5.

Muda wa Kuhifadhi rafuni (shelf life):
Matunda yanaweza kuhifadhiwa vizuri katika sehemu yenye kivuli, hewa inayozunguka vizuri na joto la kawaida kwa wiki 1 mpaka 2, waweza pia kuhifadhi kwa wiki 4 mpaka 5 katika nyuzi joto 7, ila zingatia baridi ikizidi sana yaweza kusababisha mashambulio ya fangasi.

FAIDA ZA KARAKARA
- Mbegu zake hutoa mafuta (23%) yanayofanania na ya Alizeti.
- Majani yake hutumiwa sehemu mbalimbali kama dawa kupunguza shinikizo la damu, kansa na kadhalika.
- Maua yake hutumika kutibu mfumo wa akili, mapafu, asthma na kadhalika.
- Ni chanzo kikubwa cha vitamin C, madini ya chuma na virutubisho vinginevyo.
- Juisi yake ni moja ya viburudisho maarufu na bora sana hasa kwa ladha yake na kunukia kwake vizuri.

KWA MAELEZO ZAIDI WASILANA NASI


  • +255 764 191 170 Mr Mpinga


MBEGU BORA ZA TIKITI, VITUNGUU, NYANYA, HOHO, N.K 

kilimoforlife@gmail.com

Maoni

  1. Asante kwa uchambuzi makini, Mungu akubariki

    JibuFuta
  2. Asante kwa uchambuzi ila baadhi ya vitu mbona umeficha?

    JibuFuta
  3. Asante kwa uchambuzi ila baadhi ya vitu mbona umeficha?

    JibuFuta
  4. Asante kwa uchambuzi ila baadhi ya vitu mbona umeficha?

    JibuFuta
  5. Nusu Hekta ni 50×50? Square Meter 2500 ni Nusu Hekta? Mimi nafahamu nusu hekta ni square meter 5000

    Tafadhali rejea vyema vipimo.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho Maarufu