kilimo bora na cha kitaalamu cha mahindi nchini Tanzania


KILIMO BORA CHA MAHINDI.

Related image

Habari mpendwa msomaji wamakala zetu za kilimo for life, naamini ubuheri wa afya.
Kama ilivyo kawaida yetu kukujulisheni juu ya kilimo cha mazao mbalimbali hasa yanayolimwa nchini Tanzania, leo ningependa tujionee ni jinsi gani ya kukiendea kilimo bora cha mahindi kwa mavuno mengi na yenye faida kwa mkulima.
Mahindi ni zao linalolimwa zaidi nchini Tanzania kwani ni zao kuu la chakula kwa watanzania takriban wote waliomo nchini.

HALI YA HEWA.
Mahindi hustawi vyema katika ukanda wa 2500 m kutoka usawa wa bahari, hali ya joto ridi la wastani ni 20 o  na joto ridi la juu zaidi kwa zao la mahindi kustahimili ni nyuzi joto 30o.
Ili kukuwa vyema zao la mahindi  linahitaji mvuwa za kutosha kwa kiwango cha 450 mm hadi 650 mm kwa msimu.
Pia zao la mahindi linahitaji ardhi na udongo wenye rutba na kiwango cha tindikali cha 6 hadi 6.5, udongo usio na chumvi, udongo wa kichanga tifutifu  usio tuamisha maji kwa muda mrefu ni udongo mzuri zaidi kwa mahindi.
Zao la mahindi hukomaa kwa muda wa siku 75 hadi 125 kulingana na aina ya mbegu, na zao la mahindi huhitaji zaidi mvuwa za awali hadi kipindi cha kuchanuwa. hivyo ni vyema mkulima akachaguwa mbegu kulingana na ukanda wake wa ekolojia.

Mbegu  za mahindi
kwa mkulima yeyote wa mahindi duniani hana budi kuzingatia matumizi ya mbegu bora kwa uhakika wa upatikanaji wa mavuno mengi na bora.


Mambo ya kuzingatia katika kuchaguwa mbegu ya mahindi
·         Mkulima achaguwe mbegu ya mahindi yenye uwezo wa kutoa mavuno mengi.
·         Mkulima azingatie mbegu zenye uwezo wa kustahimili magonjwa na visumbufu mashambani.
·         Mbegu yenye kutoa mahindi yenye ubora katika lishe (mahindi mengi siku hizi yana pumba nyingi kuliko viritubisho).
·         Kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa mkulima hana budi kuchaguwa mbegu yenye  kustahimili ukame.

Ushauri wa matumizi ya mbegu zilizoboreshwa unatofautiana kutoka eneo moja na lingine kwa sababu ya:

  • Mwinuko kutoka usawa wa bahari
  • Kiasi cha mvua katika eneo husika
  • Muda unaotumia mbegu hadi kukomaa
Bonyeza hapa kufahamu mbegu zilizoboreshwa kulingana na ukanda nchi Tanzania.

UTAYARISHAJI WA SHAMBA.
Shamba la mahindi linapaswa kutayarishwa mapema iwezekanavyo kabla ya msimu wa mvuwa haujaanza rasmi.
Teketeza mabaki ya mahindi katika shamba lililoathiriwa na magonjwa au wadudu waharibifu kama vile kiwavi kijeshi vamizi ili kupunguza au kuzuia uwezekano wa kuibuka upya na zaidi wa ugonjwa au mdudu huyo.
Kwatuwa/ lima shamba lako na hakikisha unatifuwa udongo vizuri zaidi kwa kwenda chini sentimita 15-25 ili kuruhusu upenyaji mzuri wa mizizi.

Upandaji wa mahindi
Mkulima anapaswa kuzingatia kanuni zifuatazo katika upandaji wa mahindi.

Muda wa kupanda: 
Mkulima apande mahindi Kulingana na msimu wa mvuwa ampapo maeneo mengi nchini Tanzania mvuwa huanza mwezi  November na mikoa mingine mvuwa huanza mwezi Februari.  Hivyo mkulima ni vyema akapanda wiki mbili kabla ya mvua kuanza rasmi.
  • MUHIMU: Ni vyema wakulima kuzingatia taarifa za mamlaka yahali ya hewa nchini.
Namna ya kusia mbegu  ya mahindi shambani.
Mkulima anashauriwa kufuata kanuni za upandaji wa mahindi kitaalamu kama itakavyo ainishwa hapa chini.

Image result for maize planting spacing
Shimo
sia mbegu ya mahindi katika shimo lenye kina cha sentimita 3 hadi 5 kwenda chini.

Nafasi
Mkulima anapaswa kuzingatia nafasi baina ya mahindi pindi anaposia mbegu ya mahindi.
Kupanda kwa nafasi ni kati ya njia bora za kilimo inayomwezesha mkulima kupata mazao bora. Hivyo ni muhimu sana kuzingatia kupanda mbegu kwa mistari na kufuata nafasi zinazoshauriwa kitaalamu katika kilimo. Zifuatazo ni nafasi za kupanda mahindi na idadi ya mbegu kwa kila shimo na kiasi cha mbolea ya kupandia inayo takiwa kuwekwa katika shimo:

  • Kwa nafasi ya 75 sm X 30 sm, panda mbegu moja katika shimo.
  • Kwa nafasi ya 75 sm X 25 sm, panda mbegu mbili katika shimo.
  • Mbolea ya kupandia mahindi.
Image result for dap mbolea

Mkulima anashauriwa kutumia mbolea yenye fosforasi kabla ya kupanda. Mfano DAP, minjingu,MOP, TSP au Yaramila otesha.

Kiwango cha mbolea ya kupandia
Tumia kijiko kimoja cha chakula kuweka mbolea katika kila shimo.
 
Kupalilia
Ni muhimu shamba la mahindi lipaliliwe siku 14 hadi 21 baada ya mimea kuota kufuatana na hali ya shamba wakati wa kupanda. Wataalamu wanashauri kwamba katika kilimo cha mahindi, shamba lipaliliwe mara 2.
Magugu ni hatari zaidi katika shamba la mahindi kwani  yanaweza kupunguza mavuno kwa asilimia 60 hadi 100 kadiri palizi linavyocheleweshwa shambani. Magugu hushindania virutubisho na pia kuhifadhi wadudu na magonjwa yanayoweza kushambulia mimea iliyopandwa na hivyo kupunguza mavuno zaidi. Palizi hufanyika kwa namna mbalimbali kama palizi ya mkono kwa kung’olea (ikiwa magugu yapo mbali mbali sana) au kulima kwa jembe la mkono au kwa kutumia viuagugu (herbicides) mfano 2-4D.


Mbolea ya kukuzia mahindi
mbolea ya kukuuzia ni muhimu sana kwani huharakisha ukuaji na ukomaaji wa mahindi shambani, husaidia mmea kustahimiliukame na magonjwa pia husaidia mahindi kutoa mahindi yenye ubora kipindi cha mavuno. Mbolea ya kukuuzia huwekwa mara baada ya mmea kufikia urefu wa sentimita 40 hadi 50. Na mbolea  ya kukuuzia ni lazima iwe na kiwango cha kutosha cha nitojeni.
zifuatazo ni mbolea za kukuzia  mahindi ni NPK, UREA, CAN, S A na Yaramila winner.
Image result for NPK, CAN, YARAImage result for NPK, CAN, YARA

Pia wakulima hutumia mbolea za kukuzia zinazopatikana kwa bei nafuu kama vile BOOSTER (foliage nitrogeneous fertilizers) ambayo hupigwa kwa kunyunyizia katika majani ya mmea kila baada ya wiki 3, kwa mara 2-3 mpaka mahindi kuvunwa. Kiwango cha kupiga ni mchanganyo wa mls 50-80 ktk lita 15 za maji.
 Mbolea za kukuzia huwekwa kuzunguka kila shina la mimea au pande mbili au tatu au nne za kila shina. Kiwango cha matumizi ya mbolea mkulima ni bora akashauriwa na bwana shamba wake kulingana na hali ya udongo katika shamba.

KUVUNA, KUKAUSHA, KUSAFISHA NA KUHIFADIHI
 Kuvuna

Image result for Dried maize plant
Mahindi hukoma kwa muda wa takriban siku 75 hadi 125 kutegemea na aina ya mbegu na hali ya hewa. Kuna baadhi ya mbegu huwa ni za muda mfupi na nyingine huwa ni za muda mrefu, pia ikumbukwe kuwa maeneo ya ukanda wa baridi kali huwa ni sababu ya kuchelewa kukomaa kwa muhindi.
Mahindi huwa tayari kwa kuvuna  pindi kikonyo kimekuwa dhaifu na hugeuza  mahindi kuangalia chini.

KIWANGO CHA MAVUNO.

Kwa mkulima atakaetumia mbegu chotara mfano AGRISEED H12, MERU F1, PANNA nk. mavuno ya chini kabisa huwa ni gunia 20 za kilo 100. Na mavuno ya juu kabisa huwa ni gunia 32 kwa ekari.

Kwa mkulima atakaetumia mbegu zilizoboreshwa mfano SITUKA M1, STAHA nk: mavuno huanzia gunia 10 na mavuno ya juu kabisa huwa ni gunia 16 za kilo 100 kwa ekari moja.

Kukausha
Ni muhimu mahindi yakauke vizuri ili yasioze au kubunguliwa na wadudu kirahisi yakiwekwa ghalani. Ili kujua kama mahindi yamekauka vizuri, tia mahindi kadhaa kwenye chupa ya soda iliyokauka na uongeze kiganja kimoja cha chumvi. Tingisha chupa halafu uwache itulie kwa dakika tatu. Chumvi ikikwama kando ya chupa, basi mahindi hayajakauka vizuri.

kupukuchuwa.
Kitendo cha kutenganisha punje za mahindi kutoka katka gunzi. Mahindi hupukuchuliwa kwa njia ya mikono, kupigwapigwa kwa mipini au kwa njia ya mashine ya kupukuchulia.

Kusafisha
Kusafisha mahindi ni muhimu ili kuondoa uchafu na mahindi yaliyoharibika ambayo yanaweza kukaribisha wadudu ghalani.
Mahindi yaliyokauka vizuri hupepetwa na vilevile mahindi mabovu hutenganishwa. Hii hufanyika kwa kutumia vifaa vya majumbani kama vile ndoo, ungo na mabeseni au kutumia mashine pindi mahindi yanapopukuchuliwa.

Kuhifadhi
Ni muhimu kuhifadhi mahindi mahala pazuri pasipo kuwa na joto kali, pawe pakavu, pasivujiwe na maji na pasiingiwe na wadudu kirahisi.
Mahindi huhifadhiwa ghalani baada ya kuwekwa viatilifu vya kuzuia bungua wa mahindi Njia za kisasa za uhifadhi hutumiwa kama vile matumiz ya ACTELLIC SUPER DUST katika uwiano wa 1kg kwa gunia 5-10 za ujazo wa 100kg. Kiatilifu kingine ni actellic solution katika rate ya 5mls katika gunia moja la kg 100. Njia nyingine ya kienyeji katika kuhifadhi mahindi ni kuweka juu ya ghala ambalo chini yake kuna jiko la kupikia ambalo hutoa moshi unaotumika kufukuza na kuua wadudu.
Image result for actellic 300cs
WASILIANA NAMI KWA USHAURI WA KILIMO CHA MAZAO YOTE.
+255 757 139 423 Mr MPINGA
kilimoforlife@gmail.com

Maoni

Machapisho Maarufu